Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saumu Heri Sakala

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SAUMU H. SAKALA (K.n.y. MHE. MUSSA B. MBAROUK) aliuliza:- Awamu zote za Serikali zilizopita Awamu ya Kwanza, Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne ziliahidi kujenga barabara ya Tanga – Pangani – Saadani hadi Bagamoyo kwa kiwango cha lami:- (a) Je, ni lini Serikali itaamua kujenga barabara ya Tanga – Pangani kwa kiwango cha lami? (b) Kupitia Bunge la Kumi na Moja, je, Serikali inaahidi nini kuhusu ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Anaitwa Mussa Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kutambua umuhimu wa barabara hii ambayo ina kivutio cha pakee ambacho imeunganika na mbuga pamoja na bahari. Je, Serikali kwa kuendelea kuchelewa kuitengeneza barabara hii kwa kiwango cha lami, haioni kuwa inapoteza mapato mengi ya kiutalii kutokana na kivutio hiki? (Makofi)
Swali la pili, Wakazi wa Wilaya ya Pangani ambao wako pembezoni mwa barabara ile wamewekewa alama ya “X” nyumba zao, lakini bado wanaendelea kuishi na hawajui ni lini watalipwa fidia zao ili waendelee na maisha yao sehemu nyingine.
Je, Serikali ipo tayari kutoa ahadi kwamba ni lini itawalipa wakazi hawa fidia zao? Ahsante

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali hii ya Awamu ya Tano inapotoa ahadi inatekeleza; barabara hii imeanza kufanyiwa usanifu na itakapokamilika maadam tumeshaona mtu anayetoa fedha tayari amepatikana kwa vyovyote vile ujenzi utafanyika kwa haraka itakavyowezekana ili mapato haya ya kitalii yaanze kuingia katika Mfuko wa Hazina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali la pili, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, hizo alama za “X” anazoziona ndiyo sehemu ya utaratibu wa kufanya fidia. Ni hatua ya kwanza, baada ya hapo wanamalizia hatua inayofuata na mara utaratibu wa kufanya uthamini utakapokamilika suala la ulipaji wa fidia litashughulikiwa.