Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO K.n.y. MHE. TABASAM H. MWAGAO aliuliza: - (a) Je, ni lini Jimbo la Sengerema litapata Kivuko kipya angalau kimoja kati ya vivuko vitano ambavyo Serikali imepanga kujenga katika Ziwa Victoria kwa bajeti ya mwaka 2021-2022? (b) Je, Serikali inafahamu adha ya usafiri wanayoipata wananchi wa Mji Mdogo wa Buyagu Wilayani Sengerema pamoja na wananchi wa Wilaya za Misungwi na Nyang’hwale kwa kukosa chombo madhubuti cha usafiri wa majini?

Supplementary Question 1

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa ninalo swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo la Buyagu sasa linaelekea kufikia hatma, lakini bado wananchi wa Kata ya Ilunda Wilayani Sengerema wana adha ya namna hiyo ya kuwa na kivuko kidogo: Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka kivuko kikubwa katika eneo hili la Ilunda? (Makofi)

Mheshmiwa Naibu Spika, swali la pili: Kwa kuwa Wilaya ya Sengerema inayo majimbo mawili; lipo Jimbo la Buchosa na Mheshimiwa anafahamu kwamba watu wa Kome, Nyakalilo, Nyakasasa, Mtama wana matatizo makubwa ya usafiri: Je, Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka kivuko kikubwa katika maeneo haya? (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shigongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza katika eneo la Sengerema – Buchosa wana bahati kwamba tunajenga daraja kubwa pale Kigongo – Busisi na kuna vivuko kadhaa vinafanya kazi katika Ziwa Victoria. Baada ya barabara hiyo na daraja kukamilika, maana yake vivuko vile vitahamishwa kwenda maeneo mengine; na maeneo haya ambayo Mheshimiwa Mbunge anataja ndiyo sehemu mojawapo tunaenda kumaliza changamoto hii ili kuweza kutoa huduma katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyozungumza sasa tunajenga kivuko kipya ambacho kitafanyakazi Kata Nyakarilo na Kome kitaenda katika eneo hilo. Vile vile tunafanya ukarabati wa kivuko cha MV. SabaSaba ili kiende kusaidia MV2 Kome kuweka huduma katika eneo hilo. Kwa hiyo, naomba nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ipo makini sana kupeleka vivuko kwa sababu mbili; moja, ni sehemu ya biashara na pili, ni sehemu ya kutoa huduma. Watupe subira kazi zitakamilika na shida ya usafiri katika eneo hili kwenye visiwa mbalimbali Ziwa Victoria itakuwa imekamilika. Ahsante. (Makofi)