Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: aliuliza: - Kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya Taasisi za Serikali kutotumia huduma za Shirika la Bima la Zanzibar kwa kisingizio kuwa shirika hilo siyo la Umma. (a) Je, Serikali inalitambua shirika hilo kama la Serikali au shirika binafsi? (b) Kama ni shirika la Serikali, nini wito wa Serikali kwa watendaji ambao wamekuwa wakikataa kutumia huduma hiyo kwa kisingizio cha kuwa siyo shirika la Serikali?

Supplementary Question 1

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naishukuru Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Muungano kwa niaba ya Waziri wa Fedha kwa majibu mazuri ambayo nafikiri sasa yataielekeza nchi yetu kuwa shirika hili ni la Serikali kwa mujibu wa sheria.

Swali langu ni moja tu kwamba kwa vile Serikali imeelekeza taasisi za Muungano na taasisi zote za Serikali kutumia Shirika la Bima la Taifa sasa kwa nini Serikali hairudi na kuelekeza wananchi wake ili waelewe kwamba Shirika la Bima la Zanzibar ni Shirika la Kiserikali na wana wajibu pia wa kutumia kulingana na huduma zao wanakavyoona ni nzuri na mimi nikiwathibitishia wabunge kwamba huduma hizo ni nzuri? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Najma kwa juhudi yake ya ufuatiliaji wa kero za wananchi na kwa namna anavyopambana kwa wananchi wote, kwa kweli naomba hili tulichukue kama ni wazo, ni ushauri na tutalifanyia kazi. Tutashauriana na Serikali kulifanyia kazi jambo hili, ahsante.