Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Kwa muda mrefu wananchi wa Busokelo wamekuwa wakikumbana na adha kubwa ya ubovu wa barabara ya Katumba - Mbando - Tukuyu yenye urefu wa kilometa 82 inayoanzia Katumba (RDC) kupitia Mpombo, Kandete, Isange, Lwangwa, Mbwambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) na barabara hii imekuwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa muda mrefu na Mkandarasi yuko eneo la ujenzi wa kipande cha kilometa kumi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha barabara hiyo kwa kujenga sehemu iliyobaki yenye kilomita 72?

Supplementary Question 1

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini pia niseme tu kwamba barabara hii katika maeneo mengi, kama ulivyokiri kwenye jibu lako la msingi kuna baadhi ya maeneo inateleza, kuna utelezi mkali. Je, Serikali ina mipango gani kuhakikisha kwamba kwa kipindi hiki cha mvua ambapo haipitiki inaweza kujengwa kwa haraka iwezekanavyo?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa tuna maeneo mengi sana katika nchi hii yenye matatizo ya mawasiliano ya barabara. Tumetoa maelekezo mahsusi kwa kila Meneja wa TANROADS Mkoa kuhakikisha kwamba muda wote wanapata taarifa wapi kuna matatizo na wayashughulikie haraka. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, maelekezo hayo yamekwenda Mkoa Mbeya na pengine nichukue nafasi hii kama walikuwa hawana taarifa sasa wamepata taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge, wakalishughulikie hilo eneo kwa kadri ya maelekezo ya jumla ambayo Mameneja wote wameelekezwa.

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Kwa muda mrefu wananchi wa Busokelo wamekuwa wakikumbana na adha kubwa ya ubovu wa barabara ya Katumba - Mbando - Tukuyu yenye urefu wa kilometa 82 inayoanzia Katumba (RDC) kupitia Mpombo, Kandete, Isange, Lwangwa, Mbwambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) na barabara hii imekuwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa muda mrefu na Mkandarasi yuko eneo la ujenzi wa kipande cha kilometa kumi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha barabara hiyo kwa kujenga sehemu iliyobaki yenye kilomita 72?

Supplementary Question 2

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kujua barabara ya Tunduma - Mpemba yenye kilometa 12 itajengwa lini na Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu barabara ile inasababisha msongamano mkubwa sana wa magari kwenye Mji wa Tunduma na wananchi kushindwa kutimiza majukumu yao. Kwa hiyo, nataka Waziri atueleze ni lini barabara hii itaanza kujengwa kwenye Mji wetu wa Tunduma haraka iwezekanavyo? Ahsante sana.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii inahitaji takwimu, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge, avute subira tuwasiliane na wataalam ili tuweze kumpa jibu lililo na uhakika.

Name

Martha Jachi Umbulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Kwa muda mrefu wananchi wa Busokelo wamekuwa wakikumbana na adha kubwa ya ubovu wa barabara ya Katumba - Mbando - Tukuyu yenye urefu wa kilometa 82 inayoanzia Katumba (RDC) kupitia Mpombo, Kandete, Isange, Lwangwa, Mbwambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) na barabara hii imekuwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa muda mrefu na Mkandarasi yuko eneo la ujenzi wa kipande cha kilometa kumi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha barabara hiyo kwa kujenga sehemu iliyobaki yenye kilomita 72?

Supplementary Question 3

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Naibu Spika ahsante sana, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Kwa kuwa kususua kwa barabara ya hizi za Busokelo inafanana sana na kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya kutoka Dodoma kwenda Babati na hasa kipande cha Mayamaya kwenda Bonga, naomba kujua Serikali inasema nini kuhusu changamoto hiyo kubwa ambayo imechukua muda mrefu na ahadi ilikuwa mwisho wa mwaka 2015 kumalizika?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba barabara ya Busokelo na anayoongelea zinafanana, lakini hii ilikuwa inaongelea matengenezo na hiyo nyingine inaongelea ujenzi. Namwomba Mheshimiwa Mbunge, anafahamu kuna Mbunge ameleta swali kuhusiana na hii barabara. Ni hivi karibuni tu tutapata taarifa kamili na tutalijibu swali linalohusiana na barabara hii ndani ya Bunge hili linaloendelea.