Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sixtus Raphael Mapunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Mji wa Mbinga ni miongoni mwa Miji inayokua kwa kasi hapa nchini, hali inayopekekea ongezeko la hitaji kubwa la huduma ya maji safi na salama:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta mradi wa uhakika wa maji safi na salama utakooweza kuwahudumia wananchi wa Mbinga?

Supplementary Question 1

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, naomba niulize swali moja la nyongeza. Mradi unaokusudiwa kujengwa au kukamilishwa Mbinga ni mradi mkubwa; na fedha zilizoainishwa ambazo zinatafutwa, Dola milioni 11.86 ni nyingi, zinaweza zisikamilike kwa wakati:-
Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kutengeneza mpanga wa dharura kwa kukarabati miundombinu ya maji ulioko sasa ili watu wa maeneo ya Frasto, Kipika, Masumuni, Lusonga, Mbambi, Bethlehemu, Luiko na Misheni waweze kupata maji safi na salama?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimwambie Mheshimiwa Mbunge, kwamba Serikali tayari imeendelea na ujenzi wa miradi ya vijiji 10 katika Jimbo la Mbinga ambapo mpaka sasa kuna mradi mmoja wa Kigonsela ambao umekamilika na watu wanapata huduma ya maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuna miradi ambayo inaendelea ikiwepo Kingirikiti, Mkako, Kihongo, na Litoha. Pia katika bajeti ya mwaka wa fedha tunaoanza tarehe moja mwezi wa saba, tumetenga shilingi bilioni 1.7 ambazo yeye mwenye Mheshimiwa Mbunge akirishikiana na Halmashauri yake, basi watapanga kuangalia vipaumbele maeneo yale ambayo ameyataja ili yaweze kupata huduma ya maji.