Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Ili kuleta ufanisi wa kimaendeleo na kusogeza karibu huduma za kijamii kwa wananchi, Serikali hugawa Wilaya na Majimbo kwa kuangalia ukubwa wa eneo, idadi ya watu kwenye eneo husika, pamoja na shughuli za kiuchumi na Wilaya ya Kilindi ni miongoni mwa Wilaya chache zinazozalisha mazao ya kilimo na biashara kwa eneo kubwa:- Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuligawa Jimbo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 6,125?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini nina swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, vimetajwa vigezo vingi sana hapa, lakini vigezo hivyo inaweza ikawa ni sababu ya kutoleta maendeleo katika maeneo husuka. Je, Serikali haioni umuhimu kwamba kigezo cha jiografia tu kinaweza kutosha kugawanya Jimbo? Ahsante.

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 75(1) mpaka (6) imezungumzia vigezo na sifa za ugawaji wa Majimbo ndani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vigezo vilivyotajwa ndani ya Katiba ni pamoja na hali ya kijografia, lakini mwaka 2010 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikwenda kufanya tafiti katika nchi za SADC na kubaini baadhi ya vigezo vingine ambavyo vinasaidia katika ugawanyaji wa Majimbo.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge katika pendekezo lako hilo, kama Serikali tunalichukua, lakini pia viko vigezo vingine vingi vya ziada ambavyo vilikuwa vikitumika katika ku-determine Majimbo yagawanywe katika mfumo upi, vingine vikiwa ni pomoja na hali ya kiuchumi, lakini settlement pattern na yenyewe huwa ni kigezo cha kuweza kutolewa ili Majimbo haya yaweze kugawanywa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pendekezo la Mheshimiwa Mbunge tunalichukua kama Serikali, lakini nimpe pia habari ya kwamba tumekuwa tukichukua na vigezo vingine ambavyo vimeainishwa katika Katiba yetu, vilevile na utafiti uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo muda wetu umebana kidogo kwa ajili ya shughuli zilizo mbele yetu. Kwa hiyo, tunaendelea na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Elly Marco Macha, Mbunge wa Viti Maalum, swali lake litaulizwa na Mheshimiwa Amina Mollel.