Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omary Ahmad Badwel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. OMARY T. MGUMBA aliuliza:- Sera ya Serikali ni kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Akina Mama kwa mujibu wa sheria ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu; lakini Halmashauri nyingi ikiwemo Morogoro Vijijini haitoi mikopo hiyo kwa makundi hayo kama ilivyokusudiwa:- Je, Serikali ina mpango gani mahsusi wa kuzibana na kuziamuru Halmashauri zote ikiwemo ya Morogoro Vijijini kutenga asilimia tano ya fedha za mapato ya ndani kwa vijana na asilimia tano kwa ajili ya akina mama ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu na kutimiza lengo lililokusudiwa?

Supplementary Question 1

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu lake la msingi Mheshimiwa Waziri amesema kwamba vikundi 39 vya vijana na akina mama wamepata shilingi 23,800,000. Nataka kujua je, fedha hizi ni kwa muda wa fedha wa miaka mingapi?
Swali la pili; fedha hizi shilingi 23,800,000 zimekwenda katika Vijiji vipi na vikundi vipi katika Halmashauri ya Morogoro vijijini? Ahsante

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza linasema pesa hizi zimeenda kwa vikundi vingapi. Ninaomba nifanye mrejeo swali hili nadhani nilijibu katika Bunge lililopita. Niliainisha vikundi hivi na nilikiri wazi nikasema kwamba pesa hizi zilizotengwa kwa Halmashauri ya Morogoro Kusini ni chache sana ukilinganisha na mahitaji halisi yaliyotakiwa kupelekwa. Nikatoa msisitizo hata katika wind up ya bajeti yetu ya Wizara ya TAMISEMI, nikasema ndugu zangu hizi pesa own source Wabunge ndiyo wenye jukumu ya kwenda kuzisimamia. Kwa sababu pesa hizi haziendi kwa Waziri wa Fedha wala haziji TAMISEMI, pesa hizi zinabakia katika Halmashauri na vikao vya Kamati ya Fedha za Halmashauri ndiyo vinavyopanga maamuzi ya mgawanyo wa pesa hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana katika bajeti yetu ya mwaka huu tukasema Halmashauri yoyote haiwezi ikapitishwa bajeti yake lazima kuonyesha mchanganuo kwa sababu hata hizi zilizopelekwa ni chache hazitoshelezi. Kipindi kilichopita nimesema hata Mkaguzi wa Hesabu za Serikali outstanding payment ambayo wapeleke karibu shilingi bilioni 39 hazijakwenda kwa wanawake na vijana. Mwaka huu peke yake tunatarajia kwamba kutokana na bajeti ya mwaka huu tumepisha shilingi bilioni 64.12 zinatakiwa ziende katika mgawanyiko huo. Lengo langu ni nini? Ni kwamba kila mwananchi, kila Mbunge atahakikisha kwamba hizo bilioni 64 tukija kujihakiki mwaka unapita katika Jimbo lake amesimamia katika vikao vyake pesa hizo zimewafikia wananchi wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni vikundi vingapi kwamba nivitaje kwa jina naomba niseme kwamba kwa takwimu nitampatia ile orodha ya mchanganuo wote wa vikundi vyote katika Jimbo la Morogoro Kusini.