Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza:- Elimu ya Afya ya Uzazi ni muhimu sana kwa vijana wa kike na kiume katika kuepuka mimba zisizo za lazima. Je, Serikali imejipangaje kuwahabarisha vijana ili kupunguza mimba zinazozuilika?

Supplementary Question 1

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo :-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kufahamu Mradi wa SITETEREKI ulileta mafanikio kiasi gani wa kubadili mienendo ya vijana baada ya tathmini? Naipongeza Serikali kwa kuandaa ajenda ya Kitaifa ya afya kwa vijana na uwekezaji.

Je, utaratibu upoje katika kufanikisha elimu kwa vijana wenye Ulemavu wa akili kwani ni kundi ambalo lipo katika makundi yenye hatari kubwa ya kuathirika pia?

Name

Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, Mradi wa SITETEREKI ulianza 2018-2019 ambao ni mradi wa miaka mitano 2018/2023 ni jukwaa la vijana ambalo linatumika kuwafikishia ujumbe vijana kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Jukwaa hilo, sehemu kubwa umekuwa ukifadhiliwa na USAID kupitia Mradi wa Tulonge Afya lakini kitaalamu Wizara ndio ilikuwa inatekeleza katika Mikoa 20 ya Tanzania Bara ambayo ilileta mafaniko ya kupunguza mimba za utotoni na kusimamia malengo ya kishule. Tathmini ya kati ya mradi itafanyika kuanzia mwezi Juni, 2020 na tathmini kubwa itafanyika mwaka 2023.

Mheshimiwa Spika, tumefanya rejea ya waelimisha rika (Pre Educators Manual) kwenye mapitio ya rejea hiyo tumeweka sura ya kuwafikia vijana wenye ulemavu ambapo tunategemea kuukamilisha hivi karibuni. Kwa kushirikiana na wadau wa Pathfinder na UMATI kuna Mtaala unaotengezwa ili kuwafikia vijana wenye ulemevu.