Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Augustino Manyanda Masele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:- Wananchi wa Wilaya ya Mbogwe wanapata changamoto kubwa katika kupata huduma za kimahakama kwa kuzifuata Wilaya za jirani:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama ya Wilaya Mbogwe?

Supplementary Question 1

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa uendeshaji wa mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bukombe kutokea Wilaya ya Mbogwe yanakuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mashahidi kutofika kutoa ushahidi kutokana na umbali, je, Serikali inaonaje ikianzisha Chamber Court Wilayani Mbogwe ili kukabiliana na changamoto hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama za Mwanzo katika Tarafa za Masumbwe na Ilolangulu na kuifanyia ukarabati Mahakama ya Mwanzo Mbogwe?

Name

Dr. Augustine Philip Mahiga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama yalivyo majibu yangu kwenye swali la msingi, ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya 33 nchini umepangwa kukamilika ndani ya miezi sita, kuanzia mwezi Juni na kukamilika mwezi Disemba, 2020. Hivyo, naendelea kumwomba Mheshimiwa Mbunge kuwa na uvumilivu ili jengo hili likamilike ambalo litatatua changamoto alizozitaja kwenye swali lake la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Tanzania imejiwekea Mpango wa kujenga na kukarabati majengo ya Mahakama kwa awamu. Aidha, Ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo katika Tarafa za Masumbwe na Ilolangulu utafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha. Ujenzi wa Majengo ya Mahakama 33 za Wilaya nchini utajumuisha Mahakama za Mwanzo katika jengo moja. Kwa mpango huo, Mahakama ya Mwanzo Mbogwe itakuwa ni sehemu ya Jengo la Mahakama ya Wilaya Mbogwe.