Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. Ramo Matala Makani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI aliuliza:- (a) Je serikali ina mpango gani wa kuboresha huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru na Katika Vituo vya Afya Nakapanya na Matemanga? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Vituo vya Afya na Zahanati katika Kata na Vijiji ili kuendana na Sera ya Afya na Ilani ya CCM?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, je, ni lini Serikali itaifanyia ukarabati miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Tunduru yakiwemo majengo yake (wodi, vyumba vya upasuaji, majengo ya mapokezi na kadhalika kwani miundombinu hiyo ni chakavu kutokana na umri mrefu tangu uhuru?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Sera ya Afya inafafanua kuhusu hitaji la uwepo wa Kituo cha Afya kwa kila Kata. Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Nampungu ambayo ni mojawapo ya kata tatu za Tarafa ya Nampungu yenye kata tatu na hakuna Kituo cha Afya hata kimoja?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Engineer Ramo Matala Makani, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi kuwa, Serikali inaendelea na mpango wa uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru ambapo wodi mbili ziko katika hatua ya ukamilishaji kwa gharama ya Shilingi milioni 140 na Hospitali imewezeshwa kufungua duka la dawa na kupatiwa mashine ya Ultrasound. Serikali itaendelea kuikarabati, kuipanua na kuiboresha Hospitali ya Halmashauri ya Tunduru kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Aidha katika Hotuba itakayowasilishwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tutatoa ufafanuzi kuhusu mpango wa ujenzi na ukarabati wa hospitali kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Mheshimiwa Mbunge anaombwa kuvuta subira mpaka wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, pili, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya ya msingi nchini kwa kukarabati miundombinu iliyopo, kukamilisha maboma na kujenga miundombinu mipya. Hadi Machi, 2020 vituo vya kutolea huduma za afya 400 ikiwemo Hospitali za Halmashauri mpya 98 zimepokea fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza hili, Serikali imetoa kipaumbele kwa maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa wa huduma za afya kwa kuzingatia vigezo vya wingi wa watu, umbali na maeneo ambayo ni magumu kufikika. Serikali inaendelea kutekeleza Sera na Mpango huu kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.