Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Ally Yusuf Suleiman

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mgogoni

Primary Question

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF aliuliza:- Mfumo wa Mahakama umejiwekea utaratibu wa kuanza na kuamaliza mashauri ambapo kwa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu ni miaka miwili, Mahakama za Mahakimu Wakazi ni mwaka mmoja na Mahakama za Mwanzo ni mie zi sita. Utaratibu huu ni mzuri ambao unaendana na msemo usemao: “Haki iliyocheleweshwa ni sawa haki iliyonyimwa.” Je, ni kwa nini utaratibu huu haufuatwi na badala yake kesi nyingi zinachukua muda mrefu?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Mheshimiwa Spika, moja ya kesi ambayo inavuta hisia ya watu wengi ni kesi ya Mashehe wa Uamsho kutoka Zanzibar ambayo ilianza awamu iliyopita na kurithiwa na awamu hii. Sasa ni zaidi ya miaka saba na hata kuanza bado:-

(a) Je, ni sababu gani iliyosababisha ucheleweshaji huu mkubwa wa uoaji haki?

(b) Je, ni muda gani kesi iliyokosa ushahidi inatakiwa kufutwa?

Name

Dr. Augustine Philip Mahiga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kesi anayoiuliza Mheshimiwa Mbunge bado ipo Mahakamani na hivyo kwa mujibu wa Kanuni za kudumu za Bunge, suala lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kujadiliwa Bungeni. Ni vyema tukasubiri vyombo husika vikafanya kazi yake na kutoa maamuzi.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, zipo sababu zinazoweza kusababisha ucheleweshaji wa kukamilika upelelezi wa kesi ya jinai, nazo zinaweza kutokana na sababu zifuatazo:-

(i) Asili na namna kosa lilivyotendeka na wahusika wanaotuhumiwa kutenda kosa hilo iwapo wametenda kosa hilo wakiwa maeneo mbalimbali kwa maana ya kuwa hawakai eneo moja na wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

(ii) Aina ya kosa husika, mathalani kesi yenye viashiria vya ugaidi, utakatishaji fedha, uhujumu uchumi, rushwa na kadhalika. Watu wanaofanya makosa ya aina hii wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

(iii) Upelelezi kuhitaji upatikanaji wa taarifa, nyaraka na mashahidi nje na ndani ya nchi. Katika mazingira hayo upelelezi wake huchukua muda mrefu kukusanya ushahidi huo.

(iv) Mheshimiwa Spika, kesi ambayo haina ushahidi haiwezi kufikishwa Mahakamani. Hata hivyo, kutokana na uzito wa kosa la kesi iliyo katika hatua za upelelezi, kesi hiyo inaweza kukaa muda mrefu katika hatua hiyo kabla ya kuamua vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwepo changamoto za ukusanyaji wa ushahidi ndani na nje ya nchi wa kesi hii, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa sasa hivi taratibu za upelelezi wa kesi hii zinahitimishwa na hivi karibuni hatua za kusikilizwa kwa kesi hii zitaanza.