Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Felister Aloyce Bura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:- Serikali ilipata ufadhili wa kujengewa uwanja wa michezo Mkoani Dodoma kutoka Serikali ya Morocco. Je, ni lini uwanja huu wa Michezo utaanza kujengwa?

Supplementary Question 1

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu Mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya Nyongeza. Kwa kuwa Mfalme wa Morocco alikubali kujenga Uwanja wa Michezo wa Kimataifa hapa Dodoma:

Je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari kuwasiliana na Serikali ya Morocco ili ujenzi uanze mapema iwezekavyo?

Kwa kuwa Dodoma ndiyo Makao Makuu: Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga viwanja vingine vya michezo ili ikiwezekana Tanzania ije ipate nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Michezo ya Kimataifa.

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika swali la msingi, mawasiliano baina ya Serikali mbili za Tanzania na ile ya Morocco yanaendelea na ni tumaini letu kwamba muafaka utafikiwa mapema iwezekanavyo kuhusu mradi huu wa ujenzi wa uwanja wa Dodoma.

Mheshimiwa Spika, pili, kwa kuwa bado mpango wa kujenga uwanja mpya wa Dodoma unaendelea, Mheshimiwa Mbunge avute subira kwa sasa Serikali ikamilishe kwanza mradi huo na kisha Serikali itaweza kufikiria kujenga viwanja vingine zaidi na siyo lazima iwe Dodoma pekee, bali hata miji mingine inayozunguka Makao Makuu ya nchi itafikiriwa.