Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Justin Joseph Monko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Mifugo ya Wafugaji wakubwa hapa nchini imekosa ubora wa mazao yake kutokana na maradhi ya nayo changi wa na kuko sekana kwa wataalam waliobobea katika fani na kukosa Maabara za Mifugo:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza wataalam ama vitendea kazi kama njia mbadala ya kuwasaidia wataalam wachache waliopo kutoa huduma bora kwa wafugaji? (b) Je, ni lini Serikali itajenga maabara za mifugo katika maeneo ya wafugaji ili wananchi waache kutibu mifugo yao kwa kubahatisha?

Supplementary Question 1

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi ambazo Mheshimiwa Waziri amezieleza, kukosekana kwa miundombinu ya uogeshaji wa mifugo kumechangia katika kudumaza afya za mifugo na uboreshaji wa majosho nchini umekuwa kwa kasi ndogo sana:-

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa muda mfupi wa kuboresha majosho nchini katika maeneo ya wafugaji?

(b) Wizara ina mkakati gani wa kuhakikisha chanjo hizi muhimu zinapatikana kwa urahisi wakati wote?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020 jumla ya majosho 292 yamekarabatiwa nchini. Kati ya hayo, 161 yamekarabatiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na 131 yamekarabatiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Majosho hayo yapo katika mikoa ya Singida, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Mara, Mwanza, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu na Tabora.

Aidha, Wizara imetoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kukarabati miundombinu ya mifugo yakiwemo majosho kwa kutumia fedha inayotokana na mapato ya ndani kutoka katika Sekta ya Mifugo.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara imetenga kiasi cha shilingi 100,000,000/= kwa ajili ya kukarabati majosho 125 katika Halmashauri za Wilaya 25 ikiwemo Singida.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kuimarisha uzalishaji wa chanjo ndani ya nchi ambapo uzalishaji wa aina za chanjo katika Kiwanda cha Kuzalisha Chanjo za Mifugo (TVI) cha Kibaha umeongezeka kutoka chanjo aina nne mwaka 2018/2019 kufikia chanjo aina sita kwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, aidha, jumla ya dozi 49,008,325 za chanjo zikiwemo dozi 47,347,700 za chanjo ya matone dhidi ya Ugonjwa wa Mdondo (TEMEVAC - I ), dozi 626,000 za Ugonjwa wa Kimeta, dozi 113,000 za Ugonjwa wa Chambavu, dozi 756,600 za Ugonjwa wa Mapafu ya Ng’ombe, dozi 19,275 za Ugonjwa wa Kutupa Mimba na dozi 145,750 za chanjo zenye muunganiko wa Kimeta na Chambavu (combination of Blackquarter vaccine and Anthrax vaccine - TECOBLAX) zimezalishwa na kusambazwa kwa wadau nchini.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa utaratibu wa manunuzi ya chanjo kwa pamoja (Bulk Procurement) ambapo chanjo zote ambazo hazizalishwi hapa nchini zitaingizwa nchini ikiwemo chanjo za Magonjwa ya Mapele, Ngozi, Miguu na Midomo kwa pamoja na zitakuwa na bei elekezi na zitasimamiwa na Serikali ili kupunguza gharama ya chanjo kwa wafugaji.

Mheshimiwa Spika, aidha, kwa Mkoa wa Singida chanjo zinapatikana katika Kituo cha TVLA Kanda ya Kati kilichopo Dodoma.