Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula kama mahindi na mpunga?

Supplementary Question 1

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Pamoja na majibu ya Serikali ya kuonesha masoko mbalimbali nje ya nchi, lakini ukweli tu ni kwamba Serikali hii imekuwa ikizuia sana wafanyabiashara wanaopata masoko nje kwa kisingizio kwamba kuna njaa na haijawahi hata siku moja kuweka mpango wa kufidia hasara ambazo zinatokana na zuio hilo la Serikali.

Sasa Je, Serikali imejiandaa namna gani kuhakikisha kwamba inawapa taarifa wakulima hawa na wafanyabiashara kwamba haya masoko yapo kwasbaabu Bunge sasa hivi haliko live?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili; Mheshimiwa Waziri amesema kwamba kuna mpango wa stakabadhi ghalani lakini katika mazao haya ambayo ni ya mpunga pamoja na mahindi hasa katika Nyanda za Juu Kusini mpango huu haujaanza kufanyakazi. Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibu huu wa stakabadhi ghalani katika mazoa ya mahindi na mpunga kwenye Nyanda za Juu Kusini?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba kimsingi ufanyaji wa biashara katika nchi yoyote ile ni lazima uende sambamba na kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi wake kwa faida ya wananchi wake. Lakini niseme tu kwamba kwa hali iliopo sasa tunacho chakula cha kutosha na nipende kuwajulisha Watanzania wote na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kwamba fursa ya kuuza mazao hayo nje ipo na pale ambapo mfanyabiashara atakwama basi aweze kuwasiliana na sisi kupitia simu zetu, kupitia mitandao ya Wizara ya Viwanda na Biashara, lakini pia Wizara ya Kilimo ambayo tunashirikiana ili kuondoa vikwazo ambavyo vinaweza kuwa vinamzuia mfanyabiashara kufanya shughuli zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili kuhusu Stakabadhi Ghalani; kimsingi ni kwmaba mfumo huo umeshaanza. Nimeshawahi kutembelea baadhi ya maeneo, kwa mfano, pale Tunduru tayari mfumo unatumika kwa masoko ya mpunga, soya pale Namtumbo na maeneo mengine, kwa hiyo niseme tu kwamba huu mfumo ni mzuri kwa sababu unamuwezesha mkulima kwanza kupeleka mazao yao kwa pamoja sehemu moja na kupata soko la uhakika lakini vilevile kuzingatia ubora unaohitajika.

Name

John Wegesa Heche

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula kama mahindi na mpunga?

Supplementary Question 2

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na mimi nilitaka kumuuliza Waziri kuhusu mazao, sisi kule Tarime tuko mpakani, kwa mfano, upande wa Kenya, tumbaku wananunua kwa bei juu na soko lipo, kahawa wananunua bei juu soko lipo, mahindi wananunua bei juu kuliko Tanzania na soko lipo na watu wa Tarime wanalima wenyewe, wanaweka mbolea wenyewe. Kwa nini mnawazuia kupeleka mazao yao kwenye soko na bei ya uhakika na wanapolipwa kwa muda?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza ni kwamba kuna mazao ya kimkakati na mazo ya chakula ya kawaida na Serikali kimsingi haijazuia kuuza tunatafuta masoko, kinachohitajika ni kufuata taratibu zinazotakiwa ili pia tuweze kuwa na uratibu mzuri wa kusema kwamba katika mwaka huu, kwa mfano, katika zao fulani tumeuza nini, kwa sababu kama hakuna uratibu maalum itakuwa hata tukiulizwa swali hatuwezi kujibu kwasababu mtu anakuwa ameuza kwa njia za panya na Serikali pia inakuwa imekosa mapato mengine ambayo yanahitajika pale inapotakiwa kutozwa katika mazao hayo.

Name

Allan Joseph Kiula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula kama mahindi na mpunga?

Supplementary Question 3

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri ametoa maelezo mazuri sana kuhusu utafutaji wa masoko ambao unafanywa na TanTrade, lakini inaonesha kwamba hizo taarifa TanTrade wanakaa nazo. Na nafikiri kwamba TanTrade wanatakiwa wazipeleke hizo taarifa kwa wahusika, kwa maana watu wetu wa vijijini ambao ndio wakulima.

Je, TanTrade wana mkakati gani wa taarifa hizo kufika zinakohitajika badala ya Wizara kujibu hapa kwa sababu hii ni Wizara sasa tunataka TanTrade ifikishe taarifa kwa wakulima?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza nimpongeze yeye pamoja na waliouliza maswali ya awali kwa jinsi ambavyo wanafuatilia suala la mazao haya na kwa manufaa ya wakulima wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba TanTrade kama Taasisi tunawataka kutoa elimu mara kwa mara, na sasa hivi pia kupitia maonesho ambayo yanategema kufanyika katika viwanja vya Sabasaba pale Temeke ni fursa nzuri na kubwa kwa wakulima kuweza kujifunza na kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na uongezaji wa thamani mazao, lakini pia kupata masoko yanayotakiwa. Kwa hiyo, nimuombe tu kwamba Mheshimiwa Mbunge na yeye mwenyewe akiwa ni sehemu yetu basi anapofanya mikutano yake aweze kuwafikishia wananchi taarifa hizi.

Name

Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula kama mahindi na mpunga?

Supplementary Question 4

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuongeza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na mazao ya chakula sisi Mkoa wa Kagera tunalima mazao ya matunda, mazao ya maparachichi. Ni Majimbo mengi ambayo wanalima mazao ya parachichi kutokana na mvua zinapatikana kwa wingi, lakini maparachichi hayo yanaozea kwenye mashamba, hawana soko la kuuza hayo maparachichi yao.

Ni lini Serikali itawatafutia soko la uhakika la kuuza maparachichi hayo? Kwa sababu nchi ya Uganda wanalima maparachichi kama sisi, lakini wanayasifirisha kuyapeleka nchi za nje. Ninaomba uwasaidie na wenyewe wananchi wa Kagera kutafutiwa masoko. Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mazao ya maparachichi na matunda kwa ujumla yanafursa kubwa sana ya kuweza kupata soko ndani na nje ye nchi na habari njema ni kwambakuanzia leo na hata kesho pale Mbeya wadau wa mazao ya matunda ikiwemo matunda na mbogamboga tupo katika kujadili namna gani ya kuweza kuongeza tija katika mazao haya na niseme tu kwamba kwa upande wa wenzetu Mkoa wa Mbeya pia wamefanya vizuri sana kuwekeza katika viwanda vya matunda hususani kwenye maparachichi.

Lakini changamoto zilizokuwa zinawakabili mojawapo ni namna ya usafirishaji wa mazao hayo mpaka nje kwa sababu imekuwa ni lazima wapeleke kwanza mpaka Kenya halafu baada ya hapo ndio yaweze kwenda nje, lakini kwa hatua tuliyonayo sasa kwa uwepo wa viwanja vya ndege ambavyo vimeimarishwa na ndege zetu katika mambo ambayo tunaenda kuyaangalia ni namna gani kunawekezwa fursa za uhifadhi ya mazao hayo ili yasiharibike mapema, lakini pia kuwa na taasisi za kitafiti ambazo zitaweza kutoa ripoti rasmi yaani accredited labs (maabara maalum) ambazo zitakuwa zimeanza kuhakiki na kuwezesha mazao yetu kuuzwa moja kwa moja nje ya nchi naamini kwamba na Mkoa wa Kagera utakuwa ni miongoni mwa wanufaika.