Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anthony Calist Komu

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. ANTONY C. KOMU aliuliza:- Serikali imetekelza mradi wa maji katika Kata ya Mbokomu lakini maji mengi yanavuja barabarani na kusababisha kukosekana kwa maji maeneo mengi ya mradi kama vile vijiji vya Korini Kusini, Kiwalaa na Korini Kaskazini. Je, kwanini Serikali isihakiki ukamilifu wa mradi huo na kufanya marekebisho ikiwa ni pamoja na kubainisha waliohusika na kasoro zitakazobainika na kuwachukuliwa hatua stahiki?

Supplementary Question 1

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, majibu ya Serikali kwa kweli ni majibu ambayo yamelenga kuuficha ukweli kwa sababu ukweli ni kwamba huo mradi baada ya kukabidhiwa ulianza matatizo hapo hapo na maji hayakutoka kabisa. Sasa baadaye Wizara ikaenda kule na ikabaini kwamba ule mradi ulijengwa chini ya kiwango na MUWASA wakakabidhiwa huo mradi wakaanza kuurekebisha na tunavyoongea sasa hivi, wameshapewa milioni 135 kwa ajili ya kuukarabati. Sasa nataka kujua hao waliofanya huo ujenzi below standard wamechukuliwa hatua gani? Hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, MUWASA wamepewa mzigo mkubwa sana kule Moshi Vijijini wamekabidhiwa Kata kama 12 kwa ajili ya kuzihudumia na zina matatizo ya miradi kama hiyo ambayo ni michakavu, ambayo imejengwa chini ya kiwango n.k lakini MUWASA wanadia kwenye Taasisi za Serikali kama Chuo cha Polisi-Moshi zaidi ya bilioni moja kwa hiyo wana tatizo kubwa sana la fedha. Nataka kufahamu kutoka Serikalini kuna commitment gani juu ya kulipwa hilo deni la MUWASA ili waweze kutuhudumia vilivyo?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anthony Komu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza ni kuhusu chanzo hicho kama kilijengwa chini ya viwango; ni ukweli usiopingika kwamba kuna miradi mingi Nchi hii ya maji hasa iliyojengwa kutoka mwaka 2010 mpaka 2015 imejengwa chini ya viwango na ipo miradi kama 88 Tanzania nzima lakini nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania kwanza wapate maji. Kama mradi umejengwa chini ya kiwango au vipi nia yetu sisi ni kukarabati Watanzania wapate maji, hilo la kwanza na ndiyo muhimu. Kwa mtazamo huo ndiyo tukatoa milioni 135 kwa ajili ya kutarabati chanzo kile na hivi tunavyoongea kazi inaendelea vizuri isipokuwa kutokana na mvua zinazoendelea kidogo kazi imepungua lakini tunaamini wiki tatu zinazokuja chanzo kile kitakuwa kimekamilika na ndugu zetu wale Watanzania wanapata maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili inayofuata sasa ni kufanya uchunguzi wa kina kuelewa kwanini vyanzo hivi vilijengwa chini ya kiwango. Uchunguzi huo tunaweza kuoina kama ilikuwa kwa bahati mbaya ama kwa nini baada ya hapo taratibu za Kisheria zitachukua mkondo wake. Hatutaki kumuhukumu sasa hivi kitu muhimu mtu yoyote ni muhimu kwanza tufanye uvchunguzi tujiridhishe.

Mheshimiwa Spika, swali la pili nasema kwamba mamlaka ya maji ya Moshi imepewa majukumu mengi ni kweli na inafanyakazi nzuri na kuna madeni ambayo idara kama za Polisi wanadaiwa na naomba nimhakikishie tu kwamba jambo hilo tunalichukua na Taasisi nyingi za Serikali zinaendelea kulipa ili kuhakikisha kwamba mamlaka hizi za maji zote zinaweza kujiendeleza au kufanyakazi kwa kiwango kinachotakiwa.