Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:- Serikali aliahidi kupeleka umeme katika vijiji vyote vya Jimbo la Mbulu Vijijini kupitia REA III kwa sababu REA II haikufanya vizuri katika jimbo hilo:- Je, vijiji vingapi vitafikiwa na umeme wa REA Awamu ya III?

Supplementary Question 1

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza pamoja na majibu aliyonipa Mheshimiwa Naibu Waziri umeme mahali ambako umekwenda kama alivyosema kwenye majibu ya swali maeneo ya taasisi na visima vya maji vimerukwa. Swali la kwanza kata za Mahitadu, Masieda, Endage Chan, Heda Chini, Getiree, Bashai, Endamillai, Rolward, Endargati, Esheshi, lini zinapata umeme?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikushukuru pia umefika kwenye jimbo langu na Mheshimiwa Waziri amefika na iko ahadi ya vijiji 22 kupatiwa umeme mwaka huu. Na leo ni bajeti ya wizara yako je, Mheshimiwa Waziri vijiji hivi na ahadi hii vipo katika bajeti hii au nitegemee nini niwaambie wananchi wa Mbulu Vijijini?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri katika maswali ya msingi ya Mheshimiwa Mbunge. Nimpongeze sana Mheshimiwa Flatei Massay Mbunge wa Mbulu Vijijini alivyofuatilia masuala ya umeme vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli zipo kata sita ikiwemo Masieda, Yaendachini pia Endagi chan pamoja na Gorand, na Esheteshi pamoja na Bashi. Zipo umbali wa takribani kilometa 15 kutoka Ngoradi na kilometa 14 kutoka Mbulu Mjini. Lakini utaratibu tunaofanya sasa wananchi wa kata hizo TANESCO pamoja na REA wameshaanza kushirikiana na utekelezaji wa kupeleka umeme katika vijiji hivyo unaanza mwezi Julai mwaka huu na utakamilika Desemba mwaka huu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge wafikishie taarifa wananchi wa Mbulu Vijijini kwamba utekelezaji wa miradi hiyo katika kata hizo utafanyika kama kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili ahadi ni lini, taasisi pamoja na maeneo mengine tuwape uhakika. Mheshimiwa Mbunge anavyofuatilia masuala ya Mbulu Vijijini anavyo vijiji 76 na kati ya hivyo tayari vijiji 32 tumevipatia umeme, vijiji vinavyobaki nikupe taarifa na tathmini ya Serikali imekamilika vyote vitapelekewa umeme ifikapo mwezi Juni, 2021.