Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY aliuliza:- Katika masuala ya Haki za binadamu Tanzania ina wajibu wa ndani na nje na kila wajibu unahitaji kuonekana wazi ili kujenga imani kwamba haki za Binadamu zinatekelezwa katika viwango vya Kisheria, Kikatiba na Kimataifa? (a) Je, Serikali itatimiza vipi matakwa haya ya ndani na nje? (b) Je, ni kiasi gani Serikali imekuwa ikijenga misingi ya usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa Haki za Binadamu ndani ya nchi?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kuniruhusu kuuliza maswali mawili ya nyongeza, la kwanza ni kwamba kwa miaka miwili sasa, kumekuwa na matokeo ya kutisha ambayo kwa kweli, si asili ya Kitanzania, yakitokea kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu ni pamoja na kutekwa, kupigwa, kuteswa, kubamiza upinzani na mambo kama hayo, Je, Serikali kwa nini haijitokezi ikasimama ikahesabiwa ili tuone kama kweli haki zinalindwa Kikatiba na Kisheria? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Kwa muda sasa takribani, pengine miaka miwili, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, haina Uongozi, na kwa hivyo pengine kuna ombwe la kutazama matukio mbalimbali ya haki za binadamu. Najua hivi sasa kuna mchakato wa kutafuta hao watu wa kujaza nafasi za Tume ya Haki za Binadamu, lakini Je, kwa nini Serikali inaachia hali kudorora mpaka Tume muhimu kama hii ikakosa uongozi kwa zaidi ya miaka miwili? (Makofi)

Name

Dr. Augustine Philip Mahiga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, matukio ambayo umeyataja, na ambayo yametokea, yanajulikana Serikalini na Vyombo husika na hasa Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama vimekuwa vikifuatilia matukio hayo. Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha, lakini kazi upelelezi na kazi ya kufatilia vituko kama hivyo na vitendo kama kama hivyo, inaweza ikachukua muda na Serikali imekubali kuchukua majukumu hayo na maswali haya yanaulizwa na wananchi kama unavyouliza, yanaulizwa pia Kimataifa na tuko tayari kutoa taarifa sahihi hapo vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vitakapokamilisha uchunguzi wa namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kuhusu uongozi wa Tume ya Haki za Binadamu, Tume ile ina Bodi tayari, ina watendaji tayari mchakato wa kumtafuta Mwenyekiti, au Mtendaji Mkuu, imekamilika na kilichobakia sasa ni kufikisha jina hilo baada ya upekuzi kukamilishwa na Vyombo vya Usalama na kuipeleka kwa Mamlaka ya uteuzi na hiyo inaweza kutokea wakati wowote, lakini kazi imekwisha kamilika na inaweza kutokea wakati wowote. (Makofi)