Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Dalaly Peter Kafumu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:- Mwaka 2018 ulikuwa msimu wa mvua nyingi sana zilizosababisha kubomoka kwa mabwawa ya maji kwenye Kata za Kinungu, Nguvumoja, Mwamashimba, Nanga, Bukoko na Mbutu na kuwaacha wananchi wa vijiji zaidi ya 24 bila maji; maeneo haya ni mbuga na hayana maji chini ya ardhi hivyo wananchi hutegemea mabwawa hayo tu. Aidha, Halmashauri ya Igunga haina uwezo wa kifedha kuyakarabati mabwawa hayo mara moja:- Je, ni kwa nini Serikali isilete mradi mkubwa wa kukarabati miundombinu ya maji katika kata hizo kuwaondolea wananchi hao tabu ya maji?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana Serikali kwa kutuletea maji kutoka Ziwa Victoria na kuhakikisha kwamba Kata tano za Nanga, Bukoko, Mwamashiga, Igunga, Mbutu na Itundulu zitapata maji, lakini nipende kuiuliza Serikali, ni lini sasa Serikali itafikisha maji ya Ziwa Victoria kwenye kata zingine zilizobaki?

Swali la pili, shida ya maji kwenye kata ambazo mabwawa au miundombinu yake iliharibika ni kubwa sana na wananchi wanateseka. Naomna kufahamu, Serikali ina- commitment gani juu ya kukarabati miundombinu hii kwa sababu majibu ya Naibu Waziri yanaonekana ni ya jumla. Ahsante.

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana, lakini kikubwa sisi kama Serikali kutokana na changamoto hii ya maji, tumeona haja ya kutumia zaidi ya bilioni 600 katika kuhakikisha tutatatuoa tatizo la maji katika Wilaya ya Igunga, Nzega pamoja na Tabora. Lakini ametaka mkakati ni lini tunakwenda kukamilisha? Mradi ule unatakiwa ukamilike mwaka 2020, Mheshimiwa Waziri ametoa agizo pindi itakapofika mwezi huu wa tisa mradi uwe umekamilika na wananchi waweze kupata huduma ya maji na sisi tutalisimamia hilo.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu swali lake la pili, kuhusu suala la fedha za ukarabati. Katika Bunge lako Tukufu, tarehe sita mwezi huu, tuliidhinishiwa zaidi ya bilioni 610 katika kuhakikisha tunatekeleza miradi ya maji, lakini katika Jimbo la Igunga tumetenga zaidi ya bilioni moja. Nimuombe sana na watalamu wetu wa Igunga waone haja sasa hizi fedha ziwe kipaumbele katika kuhakikisha zinatumika katika kukarabati miundombinu hiyo na wananchi waweze kupata huduma muhimu ya maji.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:- Mwaka 2018 ulikuwa msimu wa mvua nyingi sana zilizosababisha kubomoka kwa mabwawa ya maji kwenye Kata za Kinungu, Nguvumoja, Mwamashimba, Nanga, Bukoko na Mbutu na kuwaacha wananchi wa vijiji zaidi ya 24 bila maji; maeneo haya ni mbuga na hayana maji chini ya ardhi hivyo wananchi hutegemea mabwawa hayo tu. Aidha, Halmashauri ya Igunga haina uwezo wa kifedha kuyakarabati mabwawa hayo mara moja:- Je, ni kwa nini Serikali isilete mradi mkubwa wa kukarabati miundombinu ya maji katika kata hizo kuwaondolea wananchi hao tabu ya maji?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza, wakandarasi wengi wanaofanya shughuli za miradi ya maji kwenye Wilaya ya Tanganyika, Mradi wa Kamjela, Kabungu, Ifukutwa na Mhese, asilimia kubwa hawajalipwa fedha zao. Je, ni lini Serikali itawalipa fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha hiyo miradi?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, nikubaliane naye kwanza, ni kweli tulikuwa na madeni takribani zaidi ya bilioni 88, lakini kama unavyotambua, utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana na fedha, umepata fedha hizo zaidi ya bilioni 88 katika kuhakikisha tunawalipa wakandarasi, na hata hivyo pia tumepata bilioni 12.

Mheshimiwa Spika, nataka nikuhakikishie hata wewe katika Jimbo lako la Kongwa wakandarasi wako sasa tumekwishawalipa. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge baada ya saa saba tukutane ili tuweze ku-crosscheck ile taarifa na yeye katika wakandarsi wake katika kuhakikisha tunawalipa. Ahsante sana.