Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi wamejikuta ni raia wa nchi wanazoishi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kazi lakini si kwamba hawaipendi Tanzania:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatambua Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine ili waweze kukuza uchumi wa nchi na kusaidia ndugu zao?

Supplementary Question 1

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Mheshimiwa Waziri ametuambia kwamba wapo Watanzania zaidi ya milioni moja wanaishi nje ya Tanzania kama diaspora. Sheria ya Citizenship ya Tanzania inakataza uraia pacha. Je, ni lini Serikali ya Tanzania itabadilisha sheria hiyo na kuruhusu uraia pacha? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mwaka 2014 Serikali ya Tanzania ilitoa uraia kwa wageni waliokuwa wanaishi kama wakimbizi 150,000 nchini Tanzania. Je, Serikali haioni kwamba kutoruhusu uraia pacha tunawanyima haki Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kushiriki na kujenga nchi yao na kukaa na ndugu zao?

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimshukuru Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo kwa swali lake zuri la msingi lakini na maswali yake mazuri mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza linahusu kubadilisha sheria ili kuruhusu uraia pacha. Suala la uraia pacha ni la Kikatiba, kwa hiyo kabla hatujaongelea sheria tunapaswa kwanza tukaongelee Katiba. Mchakato wa kubadilisha Katiba bado unaendelea, pale Katiba itakapobadilika na kuruhusu uraia pacha ndipo tutakwenda kurekebisha Sheria ya Uraia Na.6 ya mwaka 1995 ili kuongeza kipengele cha kuruhusu uraia pacha.

Mheshimiwa Spika, swali la pili anasema kwamba hatuoni kwamba kuzuia uraia pacha tunanyima haki. Watanzania hawa ambao wako nje tunaowaita diaspora, bado wanaendelea kufurahia haki nyingine ambazo zimetolewa hapa Tanzania ikiwemo haki ya kuwekeza kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 na haki nyingine ambazo wangeweza kuzipata.

Kwa hiyo, tunashauri kwamba Watanzania hawa kwa hivi sasa na ambao wamefanya kazi nzuri sana kama ambavyo nimeeleza, ikiwemo kuleta misaada mingi sana katika huduma za afya na baadhi ya Majimbo kama Chakechake, Kondoa, Makunduchi, Kivungwe pamoja na Namanyere yamefaidika, bado tunaendelea kushirikiana nao na wanaendelea kufurahia haki zao kama diaspora.