Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY (K.n.y. MHE. DKT. SULEIMANI ALLY YUSSUF) aliuliza:- Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kumekuwa na ongezeko kubwa la makosa katika jamii jambo ambalo linasababisha mfumo wa utoaji haki pamoja na Mahakama kuelemewa. (a) Je, kila Jaji au Hakimu anapangiwa kesi ngapi kwa mwaka ili kupunguza mlundikano wa kesi? (b) Je, ni mambo gani kimsingi yanayosababisha mashauri kuchukua muda mrefu?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kabla ya swali la nyongeza kwanza nilitaka kusema kitu juu ya mfumo wetu huu wa Bunge Mtandao, pengine hili linafaa kurekebishwa.

Mheshimiwa Spika, muuliza swali yupo nje ya Bunge na swali limekuja hakuna access aliyopewa muuliza swali kuweza kulipata swali in advance. Kwa hiyo, nimesikiliza swali moja kwa moja bila ya kuwa na taarifa kwa sababu mwenye swali hakuwa na njia ya ku-access.

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh, hilo lilikuwa tulifanye kwa utaratibu mwingine ni kwamba tu mfumo mtandao unakupiga chenga, lakini hayo mambo yako covered kabisa. Kwamba mwenye swali Mbunge yeyote kama hayuko Bungeni analitaarifu Bunge na anataarifu ni nani amuulizie swali lake na huyo anayemuulizia swali lake anatumiwa majibu yote na kila kitu anatumiwa; kwa hiyo, hayo yote yako covered, mfumo mtandao yaani uko kisawasawa, uliza swali lako Mheshimiwa Ally Saleh. (Makofi)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, lakini mwenye swali ndio kaniambia kwamba hakuna taarifa yoyote aliyoitoa. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh, Spika akishakujulisha unamuamini Spika au unamuamini mwenye swali ambaye wala Bungeni hayupo? (Kicheko)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, nashukuru; dhana ya swali hili ni kwenye haki jamii na kwamba, issue kubwa ni kupunguza idadi ya msongamano. Mheshimiwa Waziri hapa amesema kwamba kuna tatizo la idadi ya Majaji au Mahakimu, sasa je, anafikiri katika muda gani Wizara inajipa muda gani kuhakikisha kwamba hali itakuwa inatosha kiwango cha Mahakimu, Majaji na kulingana na kasi ya matendo ya jinai?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, amezungumza habari ya moja katika tatizo ni suala la ushahidi. Je, Mheshimiwa Waziri hafikiri kwamba kuna haja sasa ya kukazia kwenye suala la kukusanya ushahidi kujaribu kutumia mbinu mpya na za kisasa zaidi ili ushahidi ukamilike na ufikishwe Mahakamani kwa wakati, ili raia waweze kupata haki?

Name

Dr. Augustine Philip Mahiga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, katika Awamu hii ya Tano tumejitahidi sana, Serikali sio tu katika kuteuwa Majaji na Mahakimu, lakini pia katika kufungua Mahakama mpya kwenye Wilaya mbalimbali. Kwa kufuata utaratibu huu inaonekena kwamba katika kipindi cha maendeleo cha miaka mitano hii mafanikio ukilinganisha kipindi cha nyuma imekuwa ni asilimia 33.5.

Mheshimiwa Spika, kwa kutazama mwelekeo huu ninadhani tutaweza kufikia hatua nzuri tukimaliza mpango huu wa maendeleo ambao tunaona unamalizika mwaka huu na tukifuata utaratibu tuliokuwa katika mpango uliopita tunaweza kufikia zaidi ya asilimia 50 kwa kuweza kukamilisha mwelekeo wa ujenzi na uteuzi katika miaka mitano ijayo.

Mheshimiwa Spika, katika suala la upelelezi na mashahidi, mfumo mzima wa Mahakama sasa hivi ni kufanya kazi kwa karibu na mtambuka na vyombo vyote vinavyofanya kazi pamoja na haki, hasa Wizara ya Mambo ya Ndani, lakini pia tumeanzisha utaratibu wa electronic ambapo tunaweza kusajili, tunaweza kupata ushahidi kwa kutumia electronic katika mikoa mitatu sasa hivi na nia yetu ni kuhakikisha kwamba mfumo huu wa electronic unaenezwa kwenye mikoa mingine. Na kwa kweli, umesaidia sana katika kuharakisha mfumo mzima wa kutoa haki ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi. Ahsante.