Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY aliuliza:- Chuo cha Diplomasia kimekuwa na umuhimu mkubwa katika masuala ya kidiplomasia na uwakilishi wa Tanzania nje ya nchi. (a) Je, Chuo cha Diplomasia kimetoa wahitimu wangapi na mgawanyiko wake ukoje hadi sasa? (b) Je, wahitimu wangapi hadi sasa wamepanda na kuwa Career Diplomats? (c) Diplomasia inaenda sambamba na mawasiliano, je, Serikali haijafikiria kuongeza lugha zinazofundishwa chuoni hapo?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika siku chache ambazo nimeridhika la jibu la Serikali, this is a very good answer from the Government. Kuna takwimu za kutosha, kuna maelezo ya kutosha. Hivi ndivyo ambavyo ningetarajia majibu ya Mawaziri wengine yawe kama haya. Nina maswali mawili ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, chuo chetu ni cha miaka mingi hivi sasa na kama uzoefu, basi upo wa kutosha: Je, Mheshimiwa Waziri katika muongo ujao, miaka kumi ijayo, anakionaje chuo chetu? Kitakuwa kimefikia hadhi na kiwango gani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kada ya wana- diplomasia ni muhimu sana, kuna ambao tunaamini kwamba chuo hiki kinapaswa kuwa ndiyo alama ya Tanzania maana Career Diplomacy na hata Political Diplomacy wote wanapita hapa ili kwenda ku-shape sera na mitizamo na namna ya kuilinda na kuitetea Tanzania.

Je, kwa kiasi gani chuo hiki kinaweza kutumika kuwa ni think tank ya kujenga sera na mikakati ya kidiplomasia ili kwenda kuitetea nje kwenye ushindani na ukinzani wa Kidiplomasia?

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote, nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Ally Saleh kwa pongezi alizozitoa kwa jibu ambalo tumelitoa. Pili, nichukue fursa hii kujibu maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza aliuliza: Je, tunakionaje chuo kwa miaka kumi ijayo? Naomba tumweleze Mheshimiwa Ally Saleh, Mbunge wa Malindi pamoja na Watanzania wote kwamba Chuo chetu cha Diplomasia ni chuo ambacho kinaheshimika sana Barani Afrika. Umeona idadi ya nchi ambazo zimeleta wanafunzi hapa na zinaendelea kuleta wanafunzi hapa, hiyo ni ishara tosha kwamba heshima ya chuo hiki ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Wizara ni kukifanya Chuo hiki sasa kivuke mipaka kwenda nje ya mipaka. Tuna makubaliano ya awali na ndugu zetu wa Argentina waweze kukitumia chuo hiki kupata elimu ya Diplomasia. Hiyo ni ishara kwamba tunavyokwenda miaka kumi ijayo, yajayo yanafurahisha zaidi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili aliuliza; je, Chuo kinaweza kuwa kama think tank? Hivi sasa kada ya Diplomasia inakuwa vizuri, tumepata wataalam wengi na sisi kama Serikali tunaendelea kuimarisha hiki chuo kwa kuweza kusomesha waatalam wengi zaidi na kuleta wengine kutoja nje kwa kupitia nyanja za ushirikiano ili kukifanya chuo hiki kiendelee kuheshimika na kitoe waatalam wengi watakaosaidia Tanzania katika Diplomasia.