Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Venance Methusalah Mwamoto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. VENANCE M. MWAMOTO (K.n.y. MHE. GODFREY W. MGIMWA) aliuliza:- Taarifa mbalimbali za kitafiti zinaonesha kwamba Mkoa wa Iringa unaongoza kwa tatizo la utapiamlo:- (a) Je, ni vigezo gani vinatumika kufikia kwenye takwimu hizo? (b) Je, jitihada gani zinachukuliwa na Serikali kunusuru tatizo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mhehimiwa Naibu Waziri naomba niulize maswali mawili. Swali la kwanza; kwa kuwa tatizo hili sasa ni kubwa na linafahamika kwa muda mrefu hususani Mkoa wa Iringa.

Je, Waziri atakuwa tayari kuja Iringa kuona hali ambayo inaendelea kwa sababu hali ni mbaya hiyo elimu ambayo ilitakiwa itolewe haitolewi kwa muda na watu wanazidi kuathirika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa shule nyingi wanakunywa uji, je, sasa haoni ni wakati muafaka sasa wa kuchanganya chakula lishe kwenye uji wao ili iwe rahisi zaidi watoto wote wakapata kwa sababu ndio wanaoathirika?

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Venance Mwamoto, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru na kumpongeza kwa kuwa ni mdau wa masuala ya lishe, lakini nipongeze vilevile Bunge lako Tukufu kwa sababu wana Chama cha Waheshimiwa Wabunge ambao wanasimamia masuala ya lishe ambacho kinaongozwa na Mheshimiwa Dunstan Kitandula, yote hii inaonesha kwamba na nyinyi kama Bunge mnalisimamia suala hili kikamilifu.

Pia kwa njia ya kipekee vilevile nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuzindua mpango mkakati wa masuala ya lishe nchini na kutoa maagizo kwa Wakuu wote wa Mikoa na kuwapa malengo ambayo ya kusimamia katika masuala haya ya lishe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niko tayari muda wowote kwenda Iringa kwenda kuwahamasisha masuala ya lishe katika mkoa huu. Vilevile ninachotaka kukisema ni kwamba hali ya udumavu tunaiona katika mikoa inazalisha chakula kwa wingi Rukwa, Katavi pamoja na Iringa ni mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa sana inazalisha chakula kwa wingi, lakini kuna udumavu mkubwa sana kuliko mikoa mingine ambayo haizalishi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, yote hii inaonesha kwamba elimu ya lishe bado ni changamoto kubwa sana na hili sisi kama Wizara tuko tayari kwenda kule kushirikiana na timu zetu za mikoa kuhakikisha kwamba tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nitumie fursa hii kutoa rai kwa jamii sasa hivi kama Taifa tunaona hali ya udumavu inazidi kupungua, lakini tumeanza kuona vilevile lishe iliyopitiliza imeanza kuongezeka, asilimia 10 ya Watanzania wana lishe ambayo imepitiliza, maana yake ni nini? Ni kwamba wote hapa wengi hatuzingatii misingi ya lishe, tunakula bora chakula kuliko chakula kilicho bora.