Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rwegasira Mukasa Oscar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Wananchi wa Kijiji cha Busiri, Wilayani Biharamulo ni miongoni mwa Watanzania ambao wanaendesha maisha kwa shughuli za uchimbaji mdogo kama ilivyo kwa wenzao wengi na kwingineko nchini. Uchimbaji mdogo wa Busiri unahitaji kuungwa mkono na Serikali kimkakati:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunga mkono wachimbaji wadogo wa Busiri na ni upi? (b) Je, Serikali ipo tayari kuwatembelea wananchi wa Kijiji cha Busiri ili kuwaelewesha ni namna gani itaanza utekelezaji wa mpango huo wa kuwaunga mkono wachimbaji hao?

Supplementary Question 1

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti ilishafanya utafiti Wilayani Biharamulo ikiwemo eneo la Busiri na ripoti ipo; na kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema STAMICO imenunua mtambo utakaosaidia wachimbaji kuongeza uzalishaji, je, Serikali iko tayari sasa kupeleka mtambo huo sambamba na kwenda na Waziri ili tukaweke mipango vizuri pale ili tuanze shughuli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Waziri amesema Vituo vya Umahiri vinaanzishwa na kwenye Mkoa wa Kagera ni mmojawapo lakini bahati mbaya siyo Biharamuro ambapo ndiko reserved kubwa ya madini ya dhahabu ipo. Je, Serikali inaweza ikatuambia ni kwa nini Kituo hicho cha Umahiri hakikuwekwa Biharamulo? Kwa sababu kuweka kiwanda cha korosho Bukoba au kiwanda cha kupaki senene Mtwara ni jambo ambalo linaweza lisiwe na tija.

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kushirikiana na STAMICO tuko tayari kabisa kupeleka mtambo huo katika maeneo hayo kwa ajili ya utafiti. Walete maombi na sisi tupo tayari kupeleka mtambo huo kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa amehoji kwa nini Kituo cha Umahiri tumekiweka sehemu nyingine na wala si Biharamuro. Kwa kweli kituo hicho tumekiweka katika Mji wa Bukoba na kitaendesha mafunzo yake katika Mji wa Bukoba kwa sababu tumeangalia sehemu ambayo ni center.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kagera ni mkubwa, tuna uchimbaji mwingine mfano wa tin kutoka Kyerwa, dhahabu kutoka Biharamuro na maeneo mengine. Kwa hiyo, pale ni center ambapo wachimbaji watakutana na ni rahisi kufika Bukoba. Kama ilivyokuwa katika huduma zingine za kimkoa kutoka wilaya mbalimbali wanakusanyika pale Bukoba. Kwa hiyo, tuliamua hivyo kwa sababu pale ni center.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, nimhakikishie tu Mheshimiwa Oscar kwamba tupo pamoja na yeye na tutakwenda na tutashirikiana naye na tufanya kazi pamoja kuwasaidia wapigakura wake. Ahsante sana.