Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI (K.n.y. MHE. EZEKIEL M. MAIGE) aliuliza:- Wananchi wa Msalala wengi wao ni wachimbaji wadogo, lakini hawana maeneo ya kufanyia kazi, maeneo mengi ya kufanyia kazi yana leseni za wachimbaji wakubwa na hawazifanyii kazi:- (a) Je, kuna leseni ngapi za utafiti wa madini zilizotolewa kwa maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala? (b) Je, ni maeneo gani Serikali inadhamiria kuyatoa kwa wachimbaji wadogo wa Msalala? (c) Je, kwa kuanzia, Serikali inaweza kuwaruhusu wananchi wafanye uchimbaji mdogo kwenye maeneo ya reef 2, Kijiji cha Kakola namba Tisa, Kata ya Bulyanhulu, Bushimangila na Msabi Kata ya Mega na Lwabakanga na Nyangalata Kata za Lunguya na Bulyanhulu?

Supplementary Question 1

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nichukue fursa hii kuipongeza Wizara ya Madini kwa uamuzi wake wa kuyagawa au kutoa leseni za wachimbaji wadogo kwenye maeneo ambayo awali yalikuwa yana leseni za utafiti za wachimbaji wakubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu ni kwamba kwa kuwa maeneo haya ambayo yalikuwa na leseni za utafiti za wachimbaji wakubwa yameshafanyiwa utafiti na Serikali ina taarifa za utafiti zinazoonesha wapi kuna madini, yako kiasi gani, yako umbali gani na kadhalika. Je, ili kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo waliopewa maeneo haya wasichimbe kwa kubahatisha na hatimaye kuingia hasara, Serikali iko tayari ku-share, kuwapatia wachimbaji hawa hizo taarifa za utafiti wa haya maeneo ili wachimbaji wadogo wawe wanachimba kwa uhakika wakijua hapa kuna madini na kuondokana na hali iliyopo sasa hivi ambapo wanachimba kwa kubahatisha na hatimaye wanapata hasara?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Selemani Zedi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kampuni kubwa na za kati ambazo zinamiliki maeneo ambayo ni ya utafiti sisi sasa hivi kama Serikali tumeamua kuyarudisha, kwa yale maeneo ambayo yalikuwa hayafanyiwi kazi, tumewarudishia wachimbaji wadogo waweze kuchimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge amehoji kwa nini tusiwape data zile wachimbaji wadogo kwa ajili ya kuzitumia kwa maana ya kuchimba bila kubahatisha. Ni kwamba Geological Survey of Tanzania (GST) ambayo iko chini ya Wizara yetu ina ripoti nyingi za maeneo mbalimbali ya uchimbaji. Tunawaomba wale ambao walikuwa tayari wameshaanza kufanya utafiti watupe zile data walizozipata katika maeneo waliyofanyia utafiti. Kwa kweli data tunazo, kwa wachimbaji wanaotaka kupata geological data au report kutoka GST waje wafuate taratibu na watapewa data hizo na waweze kuchimba bila kubahatisha waweze kujipatia tija katika uchimbaji.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI (K.n.y. MHE. EZEKIEL M. MAIGE) aliuliza:- Wananchi wa Msalala wengi wao ni wachimbaji wadogo, lakini hawana maeneo ya kufanyia kazi, maeneo mengi ya kufanyia kazi yana leseni za wachimbaji wakubwa na hawazifanyii kazi:- (a) Je, kuna leseni ngapi za utafiti wa madini zilizotolewa kwa maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala? (b) Je, ni maeneo gani Serikali inadhamiria kuyatoa kwa wachimbaji wadogo wa Msalala? (c) Je, kwa kuanzia, Serikali inaweza kuwaruhusu wananchi wafanye uchimbaji mdogo kwenye maeneo ya reef 2, Kijiji cha Kakola namba Tisa, Kata ya Bulyanhulu, Bushimangila na Msabi Kata ya Mega na Lwabakanga na Nyangalata Kata za Lunguya na Bulyanhulu?

Supplementary Question 2

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa wachimbaji wa Msalala kero zao zinafanana kabisa na kero ya Wilaya ya Nyang’hwale; nataka kujua ni lini Serikali itatoa leseni kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya Bululu, Ifugandi, Kasubuya, Isonda, Nyamalapa, Lyulu, Lubando na Iyenze ili hao wachimbaji waweze kupata hizo leseni na kuchimba ili waweze kuwa na uhakika wa uchimbaji wao na waweze kupata mikopo kutoka benki waweze kuchimba kisasa?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amar kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumetenga maeneo mengi na tumetenga maeneo makubwa, zaidi ya maeneo matano katika maeneo hayo.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama nilivyozungumza katika majibu ya swali la msingi, nimewaomba wananchi wa maeneo hayo wachangamkie hii fursa, waje waombe tuwagawie maeneo haya. Mpaka sasa hivi tuna maombi mengi ambayo tayari yamekwishatolewa na sisi sasa hivi tuko katika mchakato wa kuwagawia wachimbaji wadogo na ni maeneo ambayo ni mazuri, yana reserve ya kutosha na wataweza kuchimba kwa faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mikopo bado tunaendelea kuweka mchakato mzuri wa kuweza kufanya resource estimation katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji ili tupate uhakika wa reserve na benki ziweze kuwaamini hawa kutokana na data ambazo tunaweza kuzitoa katika geological reports zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kutoa fursa au kuwaeleza wananchi wa maeneo haya kwamba, wachangamkie fursa tuweze kuwagawia maeneo ya uchimbaji.