Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DEVOTHA M. MINJA aliuliza:- Wakati wa kampeni Mkoani Morogoro Mheshimiwa Rais aliahidi kumaliza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuhakikisha anarudisha viwanda, vilivyokufa na kuwachukulia hatua walioviua ili kurudisha ajira kwa vijana na wanawake:- Je, ni lini ahadi hiyo itatekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, lengo la Serikali kubinafsisha viwanda ilikuwa ni kuongeza ufanisi. Kuendelea kuwepo na viwanda ambavyo havifanyi kazi, Serikali haioni kama imeshindwa kutimiza wajibu wake?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, hivi kulikuwa kuna uharaka gani wa Serikali kuvitwaa viwanda hivi bila kuwaandaa wawekezaji badala yake hivi sasa viwanda vya Morogoro vimegeuka kuwa ma-godown, mahali pa kuhifadhi mbuzi na kuishi popo?

Mheshimiwa Spika, naomba kupata majibu ya maswali haya.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, Serikali haijashindwa kwa sababu kubinafsishwa kwa viwanda ni process na kuvitwaa vilevile ni process na tunapovitwaa ni lazima kuzingatia sheria, taratibu na kanuni tulizojiwekea. Kwa hiyo, tunafanya hivyo kwa kufuata taratibu zote.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la pili la uharaka gani, huwezi ukaanza kumtangazia mtu kwamba kuna kiwanda sasa kimepatikana ukichukue kabla hujakamilisha taratibu za awali za kukirejesha Serikalini.