Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Godfrey William Mgimwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. GODFREY W. MGIMWA aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Kalenga katika kata na vijiji mbalimbali wamejitolea kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati na vituo vya afya lakini hakuna wauguzi na baadhi ya vifaa tiba. Je, Serikali inaisaidiaje Halmashauri kuhusu tatizo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. GODFREY W. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante; nitakuwa nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna changamoto kubwa kwenye vituo vyetu vya afya na zahanati na changamoto kubwa ni upatikanaji wa magari ambayo yanawasafirisha wagonjwa (ambulance). Ningependa kufahamu katika vituo hivi ambavyo tunavyo katika Jimbo la Kalenga vituo kama vinne, tuna gari mbili tu lakini moja linatumika kupeleka wagonjwa katika Jimbo zima. Ningependa kufahamu, je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba tunaongezewa gari hasa katika Kituo cha Afya cha Mgama? (Makofi)
Tuna changamoto kubwa ya madawa kwenye vituo vyetu vya afya na zahanati mbalimbali hasa katika Jimbo langu la Kalenga. Ningependa kufahamu kwa sababu vituo hivi vya afya vinatumika kwa wananchi wengi. Ningependa kufahamu katika Kituo cha Ng’enza, Kituo cha Itwaga na Kituo cha Muwimbi ni lini sasa madawa yataanza kupelekwa kwa sababu kuna vituo vimeshafunguliwa kupitia mwenge lakini mpaka sasa hivi havina madawa na havijaanza kufanya kazi, ahsante. (Makofi)

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIKOA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maswali yake mawili ya nyongeza la kwanza anaulizia juu ya suala zima la upatikanaji wa gari (ambulance). Naomba nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mgimwa, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba gari zinapatikana kwa kadri hali inavyoruhusu na hivi karibuni tunatarajia kupata gari 70 na katika gari hizo 70 ambazo tunatarajia kuzipata ni matarajio ya Serikali kwamba tutalenga katika maeneo ambayo yana upungufu mkubwa sana. Nina amini eneo la kwake kama ni miongoni mwa maeneo ambayo yana upungufu mkubwa litakuwa considered.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anaulizia juu ya vituo vya afya vitatu ambavyo amevitaja kwamba vituo vya afya hivyo dawa hazipatikani. Naomba nikiri kwa fursa niliyopata ya kuzunguka katika maeneo yote ya Tanzania kwa mara ya kwanza ndiyo nasikia kwamba kuna vituo vya afya ambavyo havipati dawa. Ni vizuri tuwasiliane na Mheshimiwa Mbunge ili tujue tatizo ni nini kwa sababu ni azma ya Serikali kuhakikisha vituo vyote vinapokamilika na dawa ziweze kupatikana ili huduma iliyokusudiwa na Serikali iweze kupatikana kwa wananchi.

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GODFREY W. MGIMWA aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Kalenga katika kata na vijiji mbalimbali wamejitolea kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati na vituo vya afya lakini hakuna wauguzi na baadhi ya vifaa tiba. Je, Serikali inaisaidiaje Halmashauri kuhusu tatizo hilo?

Supplementary Question 2

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja.Kwa kuwa ujenzi wa Kituo cha Afya Mboli ambapo hata Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI Jafo anakifahamu maana ndiyo barabara yake ya kwenda Chamkoroma kule. Na kwa kuwa kituo hiki hakijakamilika wamejenga wananchi, nilikwishawaomba shilingi milioni 500 TAMISEMI ili wakamilishe kituo kile.
Je, Serikali inasemaje kuhusu kutoa shilingi milioni 500 ili tuweze kukamilisha kituo kile ili wananchi wa Kata ya Matomondo, Kata ya Mlembule, Kata ya Chamkoroma na Kata ya Tubugwe waweze kupata huduma?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikiri wazi kwamba nishukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri kwa maeneo yale ya Mheshimiwa Mgimwa ambayo ndiyo Serikali imejipanga katika utaratibu huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa swali la Mheshimiwa Lubeleje ambaye mimi namwita greda la zamani makali yale yale, si muda mrefu nilikuwa naye kule Wilayani Mpwapwa takribani wiki tatu zilizopita tulikuwa Mpwapwa. Hata hivyo kutokana na mchango mkubwa wa Mzee Lubeleje sasa hivi tunakamilisha Kituo cha Afya cha Mima na ndiyo maana siku ile alitoa hoja ya Kituo cha Afya cha Mboli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jukumu la Serikali kuhakikisha wananchi wa maeneo mbalimbali watapata huduma. Kwa hiyo, Mheshimiwa Lubeleje uwe na amani kwamba ni mpango wa Serikali kuboresha vituo vya afya na miongoni mwa vituo vya afya tutakavyoviimarisha ni Kituo cha Afya cha Mboli. (Makofi)