Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Serikali imeanzisha sera nzuri ya viwanda nchini ili kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo kwa wananchi. (a) Je, Serikali haioni upungufu wa mafundi mchundo na mafundi sadifu kuwa ni kikwazo cha ufanisi wa sera ya viwanda? (b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuziimarisha shule za ufundi za Moshi, Ifunda, Tanga na Mtwara ili kuwaandaa na kuwapatia mafundi sadifu kufanikisha sera ya viwanda nchini?

Supplementary Question 1

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa amjibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini umeona kwamba kuna utata wa maneno fundi sadifu na fundi mchundo na hilo limekuwa tatizo la elimu yetu. Fundi mchundo niartisan na Serikali imefanya vizuri sana lakini fundi sadifu ambaye ni Full Technician Certificate (FTC) holders ndio tuna upungufu mkubwa. Technical field inafanya kazi, ma-engineer wanawatelemshia hawa watu wa fundi sadifu na fundi sadifu wanawateremshia watu wa artisans.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo limekuwa tatizo, kuna gap kubwa kati ya wahandisi (engineers) wanaofanya kazi na kwenda kuunganisha huku chini nafasi katikati imepotea. Baada ya hapo nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya sana kazi ya kuanzisha Shule za Kata, zimeenea maeneo yote ya vijijini na kata. Je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kuzifanya baadhi ya Shule za Kata ziwe shule za ufundi ili kumwaga mafundi katika ngazi za vijiji na kata ili kuijenga sera hii ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imeamua kujenga VETA na kwa kuwa Jimbo langu la Tabora Kaskazini hakuna chuo hata kimoja cha VETA. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Chuo cha VETA katika Jimbo la Tabora Kaskazini.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwanza kuna vyuo vya ufundi ambavyo vinasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini pia kuna shule hizi za ufundi ambazo zimekarabatiwa kama nilivyotaja na tunaomba tupokee wazo lake tulifanyie kazi, tukiona linafaa itafanyiwa kazi na kutekelezwa ili kuongeza na kupunguza gap ambalo amelizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ameuliza kama kuna kuna uwezekano wa kuanzisha Chuo cha VETA katika Jimbo lake la Tabora Kaskazini, tunaomba tulipokee ni wazo jema likifanyiwa kazi atapata majibu kwa wakati muafaka. Ahsante.