Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Pamoja na kuwepo viwanda vingi vya sukari hapa nchini bado kumekuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo hususan kwa upande wa Tanzania Bara; mfano bei ya mfuko wa kilo 50 ni shilingi 65,000 kwa upande wa Zanzibar ambako kuna kiwanda kimoja tu cha sukari, lakini kwa Tanzania Bara mfuko huu wa kilo 50 huuzwa shilingi 120,000. (a) Je, kuna tatizo gani linalofanya sukari iuzwe bei ya juu kiasi hicho kwa upande wa Tanzania Bara? (b) Je, Serikali itachukua hatua gani ili kuweza kuwapatia wananchi unafuu katika upatikanaji wa bidhaa hiyo? (c) Kwa upande wa Zanzibar katika kipindi ambacho matumizi ya sukari kwa wananchi yanaongezeka mfano, mwezi wa Ramadhani, Serikali inashusha ushuru wa kuingia sukari nchini. Je, kwa nini Serikali ya Muungano isizingatie utaratibu huu mzuri ili kuleta unafuu kwa Tanzania Bara?

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kukiri kuwa Tanzania hakuna uhaba wa sukari katika majibu yake na amesema baada ya miaka mitatu au minne uhaba huu utapungua hiki ni kiswahili alichokiandika.
Mheshimiwa Spika, mara kadhaa tukifika katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani pamekuwa na kadhia hii ya upungufu wa sukari. Haioni Serikali imefika wakati ipunguze punguzo hili ili kuwalinda wananchi ukizingatia wananchi ndiyo waliyoweka Serikali hii madarakani na si aibu viongozi wetu Zanzibar hao Marais wetu mara nyingi ikafika mwezi Mtukufu wa Ramadhani huondoa ada hii na Tanzania Bara imeiga mambo mengi kutoka Zanzibar ikiwemo vyama vingi vimeanzia Zanzibar, haki za binadamu zimeanzia Zanzibar, matumizi ya dola yameanzia Zanzibar si aibu kuiga. (Makofi)
Je, haioni imefika wakati kuiga formula hii mara kadhaa unalinda viwanda, viwanda hivyo haviwezi kulindika wakati huu?
Mheshimiwa Spika, la pili tumo kwenye Tume ya Afrika Mashariki, lakini mpaka leo bidhaa za Zanzibar haziwezi kufika kwenye soko hilo mpaka upitie Tanzania Bara. Je, haijafika wakati Tanzania Bara mkatamka kwa Zanzibar sasa hivi isiingie katika soko hili kwa kupitia mgongo huo?

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Spika, katika jibu langu la msingi nimeeleza kwanini, sukari inayozalishwa Tanzania Bara inakuwa na gharama kubwa. Nimesema tumeamua kusimamia viwanda hivi ili tuweze kuzalisha ajira. Sasa kuhusu kupunguza nimeeleza kwamba ushuru kwa makubaliano yetu ya East Africa ni asilimia 100, tumepunguza kutoka asilimia 100 kuja 25 tumeshapunguza kuja asilimia 25. Kuhusu bidhaa ya Zanzibar kama kuna mfanyabiashara ana matatizo awasiliane na Waziri wa Zanzibar ambaye mimi na Sekretarieti inawasiliana naye. Mimi Zanzibar sina matatizo bidhaa zinakuja zinaingia nchini kama mtu hafuati viwango ana matatizo yake. Lakini TBS ya Tanzania Bara na Viwango vya Zanzibar wanawasiliana haya mambo madogo madogo myawasilishwe kwa watendaji kule na watendaji watayashughulikia, ahsante.

Name

Salim Hassan Turky

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpendae

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Pamoja na kuwepo viwanda vingi vya sukari hapa nchini bado kumekuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo hususan kwa upande wa Tanzania Bara; mfano bei ya mfuko wa kilo 50 ni shilingi 65,000 kwa upande wa Zanzibar ambako kuna kiwanda kimoja tu cha sukari, lakini kwa Tanzania Bara mfuko huu wa kilo 50 huuzwa shilingi 120,000. (a) Je, kuna tatizo gani linalofanya sukari iuzwe bei ya juu kiasi hicho kwa upande wa Tanzania Bara? (b) Je, Serikali itachukua hatua gani ili kuweza kuwapatia wananchi unafuu katika upatikanaji wa bidhaa hiyo? (c) Kwa upande wa Zanzibar katika kipindi ambacho matumizi ya sukari kwa wananchi yanaongezeka mfano, mwezi wa Ramadhani, Serikali inashusha ushuru wa kuingia sukari nchini. Je, kwa nini Serikali ya Muungano isizingatie utaratibu huu mzuri ili kuleta unafuu kwa Tanzania Bara?

Supplementary Question 2

MHE. SALIM HASSAN ABDULLAH TURKY: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuniona pamoja na majibu mazuri sana ya Waziri. Lakini katika majibu haya kuna swali la msingi ambalo Waziri naona kalikimbia, nalo ni kwamba Zanzibar kuna kiwanda cha sukari kinazalisha na kinauza sukari ile kwa shilingi 65,000 na hawaagizi sukari kutoka nje wao wamewekeza wanazalisha sukari wanauza shilingi 65,000 kwa wananchi wa Zanzibar.
Mheshimiwa Spika, swali la msingi ni kwamba viwanda vyetu vya Bara kwa nini hawawezi kutushushia bei saa hizi na ushahidi kamili ni huu ambao natoa na Bunge hili lisikie sasa hivi. Ni kwamba sukari sasa hivi katika soko la dunia linauzwa kwa bei ya dola 390, ukilipa kodi ya asilimia 25 na VAT asilimia 18 sukari hiyo inasimama kwa bei shilingi 65,000, leo Watanzania tunalanguliwa kwa kuuziwa sukari hiyo shilingi 110,000 kwa misingi gani? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na hapa hapa tuliomba cost of production ndani ya Bunge hili wakati Naibu Waziri akiwa Malima toka mwaka ule mpaka leo cost of production ya viwanda hivi hatujaletewa ndani ya Bunge hili jamani. (Makofi)

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Spika, nimejitahidi kulieleza suala hili ila muda wenyewe hautoshi. Ni kwamba gharama za uzalishaji kwa viwanda vya Bara ziko juu kuliko Zanzibar, naomba nimepewa muda, muache niwaeleze.

Name

Ally Mohamed Keissy

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Pamoja na kuwepo viwanda vingi vya sukari hapa nchini bado kumekuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo hususan kwa upande wa Tanzania Bara; mfano bei ya mfuko wa kilo 50 ni shilingi 65,000 kwa upande wa Zanzibar ambako kuna kiwanda kimoja tu cha sukari, lakini kwa Tanzania Bara mfuko huu wa kilo 50 huuzwa shilingi 120,000. (a) Je, kuna tatizo gani linalofanya sukari iuzwe bei ya juu kiasi hicho kwa upande wa Tanzania Bara? (b) Je, Serikali itachukua hatua gani ili kuweza kuwapatia wananchi unafuu katika upatikanaji wa bidhaa hiyo? (c) Kwa upande wa Zanzibar katika kipindi ambacho matumizi ya sukari kwa wananchi yanaongezeka mfano, mwezi wa Ramadhani, Serikali inashusha ushuru wa kuingia sukari nchini. Je, kwa nini Serikali ya Muungano isizingatie utaratibu huu mzuri ili kuleta unafuu kwa Tanzania Bara?

Supplementary Question 3

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, Zanzibar sukari haitoshi kwanza.

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Spika, naomba niwaeleze hili suala sio rahisi namna hiyo mnavyofikiria, ndiyo siyo suala rahisi, I am very good in talking a can talk, simple rahisi, Mheshimiwa Turky ulipopewa kibali na Serikali kuagiza sukari kwa nini wewe ukuuza bei rahisi? (Kicheko)