Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. MARTHA J. UMBULLA) aliuliza:- Mazao ya pareto na vitunguu saumu yanalimwa Wilaya ya Mbulu na yana thamani na faida kubwa kwa wananchi. Je, Serikali itakubaliana na mimi kuwa kuna haja ya kuanzisha viwanda vya kusindika mazao haya Wilayani Mbulu ili kuhamasisha kilimo cha mazao hayo?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, mazao haya ya pareto na vitunguu saumu na hata vitunguu maji ambavyo vinalimwa katika maeneo ya Mbulu na Karatu, wakulima wamekuwa wakiuza kwa vipimo vya debe badala ya kilo, na sheria ya vipimo inataka mazao haya yauzwe kwa kilo. Je, kwa nini Serikali isihakikishe kwamba mazao haya yanauzwa kwa kilo badala ya madebe?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kumekuwa pia kuna changamoto ya wafanyabiashara kufuata mazao haya shambani jambo ambalo linamfanya mkulima ananyonywa na asipate faida ya kile anachokilima, hasa mazao ya vitunguu maji ambayo yanalimwa sana kwenye Tarafa ya Eyasi, Wilayani Karatu, lakini pia maeneo ya Mbulu.
Je, Serikali sasa mna mkakati gani wa kuhakikisha kunakuwa na centeres za uuzaji wa mazao haya ili mkulima aweze kufaidika na mazao anayoyalima? (Makofi)

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Spika, kuhusu kutumia ujazo na uzito katika kupima mazao, marekebisho ya Sheria ya Vipimo Namba. 340 iko mezani kwangu na nimekataa kuisaini ilivyoletwa nikitaka twende kwa uzito, tupime kwa uzito. Nakubaliana na wewe na sitasaini mpaka wataalam wangu wakubaliane twende kwa uzito. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu vituo vya kuuzia mazao, napenda nimueleze Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote, wakulima wetu tuwahimize warudi kwenye ushirika, washikamane kuwadhibiti wale wanaokuja kunyemelea mazao. Local Government (TAMISEMI), wameshaanza zoezi la kuwa na centers ambako tutaweka mizani, lakini tukiwa na ushirika hao wanaonyemelea ambao wakulima tutaweza kuwadhibiti. Kwa hiyo, ni jukumu letu muisaidie Serikali sisi ndio Serikali twende pamoja tutaweza kuwasaidia wakulima wetu.