Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Susanne Peter Maselle

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELLE aliuliza:- Mnamo tarehe 30 Januari, 2017, wavuvi wa maeneo ya Igombe na Ilemela Jijini Mwanza walikamatwa na kunyang’anywa nyavu, mitumbwi na mashine za mitumbwi yao na Maafisa wa Uvuvi wakidai wanatumia nyavu haramu ambazo ni “double” huku Serikali ikitaka watumie “single”:- (i) Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kutoa taarifa, elimu na muda kwa wavuvi pindi inapotaka wavuvi wafanye mabadiliko katika shughuli au zana zao za kazi? (ii) Je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa wavuvi wa Igombe na maeneo mengine ya Mwanza kuhusiana na uvuvi wa kutumia nyavu za single badala ya double ili wafanye kazi zao kwa uhuru bila bughudha ya kukamatwakamatwa? (iii) Je, Serikali inataka wavuvi wavue samaki katika kina kipi cha maji na katika kina cha mita 50 na kuendelea watumie nyavu za mita ngapi kwenda chini?

Supplementary Question 1

MHE. SUSANNE P. MASELLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa nini operesheni za Serikali dhidi ya uvuvi haramu zimekuwa zikijikita katika kutekeza zana haramu za uvuvi badala ya kujikita katika kuwasaidia wavuvi hawa waweze kupata zana hizi halali kwa urahisi na kwa bei nafuu kwa kuwaondolea kodi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa uvuvi haramu unaelezwa kama moja ya tishio la kutoweka kwa samaki adimu kama ningu, nembe, gogogo, ngogwa, domodomo, sangara, njegele na sato katika Ziwa Victoria. Je, kuna mkakati wowote wa kusaidia samaki hawa kuzaliana tena ili kuendeleza fahari ya ziwa hilo na mazao yake?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini operesheni za Serikali zinajikita kuteketeza nyavu badala ya kuwapa nyavu halali? Operesheni za Serikali zinafanyika kwa mujibu wa sheria na operesheni hii inayofanyika kwa maana ya Operesheni Sangara inafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na.22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwapa nyavu za bei nafuu wavuvi ni utaratibu ambao tunao pia na ndiyo maana tumetoa punguzo la kodi na hata kuondoa baadhi ya kodi katika vifaa hivi vya uvuvi ili kusudi kuweza kuwasaidia wavuvi wetu. Kama haitoshi tumeanzisha programu maalum ambazo kwa kutumia hata Mifuko yetu ya kijamii kama vile NSSF kuwafanya wavuvi waweze kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mikopo na kuweza kununua nyavu kwa bei nafuu na vifaa vingine kwa ajili ya shughuli za uvuvi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kutoweka kwa samaki kama vile gogogo, nembe na furu. Tumeendelea kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia taasisi yetu ya utafiti ya TAFIRI ili kuhakikisha kwamba tunaendelea kulinda rasilimali hizi za nchi kwa ajili ya vizazi vya leo na vizazi vijavyo. Tunawaomba Waheshimiwa Wabunge wote waweze kutuunga mkono katika jambo hili kwa manufaa mapana ya Taifa letu.

Name

Ruth Hiyob Mollel

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELLE aliuliza:- Mnamo tarehe 30 Januari, 2017, wavuvi wa maeneo ya Igombe na Ilemela Jijini Mwanza walikamatwa na kunyang’anywa nyavu, mitumbwi na mashine za mitumbwi yao na Maafisa wa Uvuvi wakidai wanatumia nyavu haramu ambazo ni “double” huku Serikali ikitaka watumie “single”:- (i) Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kutoa taarifa, elimu na muda kwa wavuvi pindi inapotaka wavuvi wafanye mabadiliko katika shughuli au zana zao za kazi? (ii) Je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa wavuvi wa Igombe na maeneo mengine ya Mwanza kuhusiana na uvuvi wa kutumia nyavu za single badala ya double ili wafanye kazi zao kwa uhuru bila bughudha ya kukamatwakamatwa? (iii) Je, Serikali inataka wavuvi wavue samaki katika kina kipi cha maji na katika kina cha mita 50 na kuendelea watumie nyavu za mita ngapi kwenda chini?

Supplementary Question 2

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Serikali imekuwa ikichoma haya makokoro kila mara tani na tani, si muda muafaka sasa Serikali ikashughulika na wale wanaoingiza na wanaotengeneza hizi nyavu haramu nchini?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inashughulika na ndiyo maana mwaka huu mwanzoni tumekamata nyavu nyingi sana za wazalishaji wa Sunflag kule Arusha ambazo tumeziteketeza. Tumeteketeza nyavu za waagizaji kutoka nje ya nchi badala ya ku-deal na wavuvi wadogo wadogo tu. Kwa hivyo, tunashughulika na wazalishaji, waagizaji na wauzaji pia.

Name

Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELLE aliuliza:- Mnamo tarehe 30 Januari, 2017, wavuvi wa maeneo ya Igombe na Ilemela Jijini Mwanza walikamatwa na kunyang’anywa nyavu, mitumbwi na mashine za mitumbwi yao na Maafisa wa Uvuvi wakidai wanatumia nyavu haramu ambazo ni “double” huku Serikali ikitaka watumie “single”:- (i) Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kutoa taarifa, elimu na muda kwa wavuvi pindi inapotaka wavuvi wafanye mabadiliko katika shughuli au zana zao za kazi? (ii) Je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa wavuvi wa Igombe na maeneo mengine ya Mwanza kuhusiana na uvuvi wa kutumia nyavu za single badala ya double ili wafanye kazi zao kwa uhuru bila bughudha ya kukamatwakamatwa? (iii) Je, Serikali inataka wavuvi wavue samaki katika kina kipi cha maji na katika kina cha mita 50 na kuendelea watumie nyavu za mita ngapi kwenda chini?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Napenda kujua kwa nini Serikali haijikiti katika kuviimarisha Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi yaani BMU’s ili kuweza kuwa na uhakika wa uendelevu wa usimamizi wa rasilimali hizi na wenye kuleta tija? Ahsante.

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, BMUs zipo kwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na.22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake lakini pia inatambulika na Sheria ya Ugatuaji wa Madaraka kwa maana ya D by D. Sisi tunaendelea kuzitumia BMUs na katika maboresho yetu ya sheria ambayo tunayategemea kuingia katika mwaka huu tutahakikisha kwamba tunazipa nguvu zaidi na mwongozo zaidi ili BMUs ziweze kufanya kazi vile ambavyo inatakiwa kwa sababu BMUs ni mali ya wananchi wenyewe.

Name

Kasuku Samson Bilago

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELLE aliuliza:- Mnamo tarehe 30 Januari, 2017, wavuvi wa maeneo ya Igombe na Ilemela Jijini Mwanza walikamatwa na kunyang’anywa nyavu, mitumbwi na mashine za mitumbwi yao na Maafisa wa Uvuvi wakidai wanatumia nyavu haramu ambazo ni “double” huku Serikali ikitaka watumie “single”:- (i) Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kutoa taarifa, elimu na muda kwa wavuvi pindi inapotaka wavuvi wafanye mabadiliko katika shughuli au zana zao za kazi? (ii) Je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa wavuvi wa Igombe na maeneo mengine ya Mwanza kuhusiana na uvuvi wa kutumia nyavu za single badala ya double ili wafanye kazi zao kwa uhuru bila bughudha ya kukamatwakamatwa? (iii) Je, Serikali inataka wavuvi wavue samaki katika kina kipi cha maji na katika kina cha mita 50 na kuendelea watumie nyavu za mita ngapi kwenda chini?

Supplementary Question 4

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wilaya ya Kakonko ina wafugaji wa samaki waliojiunga kwenye vikundi katika Vijiji vya Nagwijima, Kasanda na Nyabibuye. Swali langu, Waziri yuko tayari kuwasaidia mikopo, ruzuku au chochote kile watu hawa ambao wametumia nguvu yao na nguvu ya Mbunge kutokana na Mfuko wa Jimbo ili waweze kuendeleza ufugaji wa samaki? (Makofi)

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko tayari kama Serikali kuwasaidia wafugaji wa samaki na ndiyo maana katika mapendekezo ya sheria na bajeti mwaka huu atakuja kuona kwamba tumependekeza kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali zinazofanya tasnia hii ya ufugaji wa samaki isisonge mbele ziweze kupunguzwa ama kufutwa ili kusudi tuweze kuwasaidia wafugaji wa samaki.