Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI aliuliza:- Katika bajeti ya mwaka 2017/2018, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Namtumbo:- (a) Je, gharama za ujenzi wa chuo hicho hadi kinakamilika ni kiasi gani? (b) Je, ni lini ujenzi wa chuo hicho utakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Wananamtumbo hawafahamu ni majengo gani yanayojengwa na wapo wanaosema kwamba linajengwa jengo la bwalo la chakula, nyumba za wakufunzi, nyumba za kulala wanafunzi, kwa hiyo wanahisi tu hawajui. Je, Serikali iko tayari kuwaeleza wananchi wa Namtumbo kwanza, hizo hisia zao kama ni sahihi na kama sio sahihi ni majengo gani yanayojengwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Profesa Ndalichako alipofika Namtumbo watu walikuja kupata taarifa baada ya yeye kuondoka na walipobeba ngoma zao kwenda kumshangilia wakakuta hayupo, je, yupo tayari hicho chuo kitakapokamilika ama yeye, kwa sababu wakimwona yeye ni sawa wamemwona Mheshimiwa Rais au kiongozi yeyote wa ngazi ya juu aje akifungue kile chuo ili wale wananchi waondoe kiu yao ya kutaka kuwaona viongozi wao wanaowapenda?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ni majengo gani yanajengwa katika ujenzi unaoendelea, naomba nimweleze Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sasa majengo ambayo yanajengwa ni jengo la utawala, karakana za ufundi seremala, uashi, bomba, umeme wa majumbani na maabara ya komputa. Majengo mengine ni pamoja na madarasa, maktaba na stoo ya generator lakini katika awamu zitakazokuja tutajenga majengo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili kama Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kwenda wakati wa ufunguzi, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa namna Serikali inavyotilia mkazo suala la ufundi na namna ninavyomfahamu Mheshimiwa Waziri anavyosisitiza masuala hayo Wizarani, nina hakika kwamba atakuwa tayari kwenda katika ufunguzi lakini hata baada ya kusikia kuna ngoma hata mimi nafikiri nitaungana naye. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.