Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. . JOSEPH R.SELASINI - (K.n.y MHE. RUTH H. MOLLEL) aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Tano inajinasibu kuzingati Utawala wa Sheria, Kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma. Hata hivyo, kuna ushahidi kuwa baadhi ya viongozi wanakiuka maadili na taratibu lakini wameachwa pasipo kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu:- (a) Je, tunaweza kujenga uchumi imara bila Watumishi wa Umma kuzingatia Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma? (b) Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Taifa linadumisha umoja ulioasisiwa na Baba wa Taifa?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH R.SELASINI: Mheshimiwa Spika, katika awamu hii umezuka mtindo kwa baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwavua vyeo baadhi ya Walimu kutokana na sababu za shule zao kutofanya vizuri, kuwavua vyeo Madaktari na hata wengine kuwaondoa kazini. Sasa mtindo huu unavyoendelea tafsiri ya jamii inaonekana kwamba ni hatua ambazo ni mahususi zilizoagizwa na Serikali. Je, Serikali iko tayari kupitia maamuzi yote haya na kuwarejeshea hao Walimu au Madaktari haki yao kama ikithibitika kwamba walionewa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, wako Walimu hasa ajira mpya na hawa wengi wako katika jimbo langu. Wanapoingia kazini hawapewi zile fedha subsistence allowance za kuwasaidia kabla hawajapata mishahara yao na nadhani hata maeneo mengine katika nchi yetu iko namna hiyo. Je, ni utaratibu gani ambao Wakurugenzi au Serikali inao wa kuhakikisha kwamba hao Walimu hawapati mateso wanapoanza kazi zao kwa mara ya kwanza?

Name

Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Mjini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Spika, ametaka kujua je, kuwavua vyeo kunakoagizwa na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Serikali iko tayari sasa kuwarudisha. Nilipojibu swali la msingi nilieleza kwamba nchi hii inaendesha kwa mujibu wa Sheria, taratibu na kanuni.
Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili ni kwamba yule aliyekuajiri wewe ndiye mwenye madaraka ya kukufukuza. Kwa hiyo, utaona kwamba mara nyingi wakigundua kwamba kuna makosa wanamsimamisha wakati wanasubiri yule mwenye madaraka ya ajira achukue hatua za mwisho.
Mheshimiwa Spika, naliomba Bunge hili kama kuna mahali mtumishi amefukuzwa na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya wakati yeye siye aliyemwajiri niletewe suala hilo nitalishughulikia mara moja, kwa sababu kwa taratibu zetu za kiutumishi yule aliyekuajiri ndiye anayekuadhibi na ndiye anayekufuza. Nimeeleza hapa jamani sisi siyo malaika, nimeeleza kwamba wakati mwingine tunapowateua tunawapa mafunzo. Hao wanaozungumzwa tumeshawapa mafunzo, naamini nadhani hata Bunge hili kama mnafuatilia maji yametulia katika mtungi siyo kama tulivyoanza huko. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili, Walimu hawapewi subsistence allowance kabla, moja nataka niseme, Wizara yangu ya Utumishi kazi yake ni kuajiri, nikishaajiri nakwambia wewe nenda Wizara ya Maji, Wizara ya Ushirika na kadhalika, sasa yule tajiri wako ndiye anayekushughulikia. Hata hivyo, siku za nyuma imetokea ilifanyika miaka ya nyuma namna hiyo, watu wakawa wanafanya ndivyo sivyo anakwenda anachukua hela anasema anakwenda kuripoti halafu haendei.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme tu kwamba kwa utaratibu tulionao sasa huingizwi wewe kwenye mfumo wa mishahara mpaka umefika, umeripoti, tuna uhakika kwamba huyu mtu kafika. Huo utaratibu unatuwezesha kupunguza udanganyifu mkubwa katika masuala ya ajira.