Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Kwa kuwa Ripoti za Ukaguzi za Ufanisi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zimeonesha kuna mapendekezo yanayotolewa baada ya ukaguzi mengi hayafanyiwi kazi na kwamba upungufu unaoibuliwa hujirudia mwaka hadi mwaka. (a) Je, Serikali inakubaliana na pendekezo la kuanzisha kitengo maalum kitakachoratibu utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi za ufanisi? (b) Je, Serikali inakubaliana na pendekezo kuwa baada ya Kamati ya PAC kujadili taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi ipeleke maoni yao kwa Kamati za Kisekta ili kutoa fursa kwa Kamati hizo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mapendekezo ya CAG hasa katika maeneo ya kisera na kiutendaji kwa mujibu wa Kanuni za Bunge?

Supplementary Question 1

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ripoti ya CAG iliyoishia Juni, 2017 imeonesha kwamba katika kaguzi zilizofanywa hasa katika Shirika la RAHCO ilitumia shilingi bilioni 20 kufanya upembuzi yakinifu wa miradi minne, lakini shilingi bilioni 20 zimepotea kutokana na kwamba miradi hiyo haikutekelezwa au haitekelezeki.
Je, Mheshimiwa Waziri atakubaliana nami kwamba kuna harufu ya ufisadi katika miradi hii minne ambayo ametumia shilingi bilioni 20 wakati ikijulikana miradi hii haiwezi kufanyika? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, imeonekana Wabunge wengi walikuwa wamelalamikia miradi ambayo inafanywa chini ya viwango ikitekelezwa na Wizara za Maji na Wizara za Ujenzi hasa TANROADS na kwamba pesa nyingi inatumika kwenye upembuzi yakinifu lakini nakuta miradi hiyo haifanywi.
Je, Serikali inakubaliana nami kwamba kuna sababu ya kumwomba Mheshimiwa Spika aunde Tume ya Kibunge ambayo itachunguza haya yote kwamba inakuwaje ifanywe miradi ya upembuzi yakinifu, lakini miradi hiyo haitengewi hela mwaka hadi mwaka? Ahsante.

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza kwamba kwenye upembuzi yakinifu wa NAFCO kwamba kulikuwa na ufisadi. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba hizi ni taarifa za kisekta na zinafanyiwa kazi na Wizara husika za kisekta. Inakuwa ni ngumu kwa mimi kusema kulikuwa na harufu ya ufisadi kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge amelitamka hili ndani ya Bunge lako tukufu; Serikali yetu ni moja, tunalifanyia kazi kuona jambo hili linafanyiwa kazi kabla ya kukiri aidha kulikuwa na ufisadi au hakukuwa na ufisadi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, nimesema kwenye jibu langu la msingi Serikali yetu hufuata Katiba, Sheria, Kanuni zikiwemo Kanuni za Bunge lako tukufu na hivyo Serikali haina mamlaka ya kulipangia Bunge nini cha kufanya. Kama Bunge lako tukufu litajiridhisha kuna umuhimu wa kuunda Tume kwa ajili ya kazi hiyo anayopendekeza Mheshimiwa Mbunge, Serikali yetu iko tayari kabisa kuona hilo linatekelezwa kwa sababu ni majukumu ya Bunge kusimamia Serikali yetu. Ahsante.

Name

Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Kwa kuwa Ripoti za Ukaguzi za Ufanisi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zimeonesha kuna mapendekezo yanayotolewa baada ya ukaguzi mengi hayafanyiwi kazi na kwamba upungufu unaoibuliwa hujirudia mwaka hadi mwaka. (a) Je, Serikali inakubaliana na pendekezo la kuanzisha kitengo maalum kitakachoratibu utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi za ufanisi? (b) Je, Serikali inakubaliana na pendekezo kuwa baada ya Kamati ya PAC kujadili taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi ipeleke maoni yao kwa Kamati za Kisekta ili kutoa fursa kwa Kamati hizo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mapendekezo ya CAG hasa katika maeneo ya kisera na kiutendaji kwa mujibu wa Kanuni za Bunge?

Supplementary Question 2

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Serikali wakati ikitoa ufafanuzi kuhusiana na kukosekana kwa taarifa za matumizi ya shilingi trilioni 1.5 ilielezwa kwamba kati ya fedha zile shilingi bilioni 200 ni makusanyo ya Zanzibar.
Sasa Mheshimiwa Waziri kabla nazo hazijatumbukia katika kero ya Muungano ni lini fedha hizi zitafika Zanzibar? (Makofi/Kicheko)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili liliulizwa wakati tukijadili bajeti ya Wizara yetu ya Fedha na Mipango na sisi kama Serikali tuliacha kulijibu makusudi kwa sababu tunafahamu mchakato wa kujadili hoja hizi za CAG ukoje, itakapokwenda kwenye Kamati ya PAC tukija hapa itajadiliwa kwa kina. Hata hivyo, naomba kusema yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi bilioni 203 ni fedha inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania Zanzibar na huwa hazivuki maji kuja Tanzania Bara. Zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti.
Naomba msikilize basi niwape elimu ili tuweze kuelewana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hizo hukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania inayofanya kazi zake Zanzibar; na zinapokusanywa fedha hizo zinasomeka kwenye financial statement za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa sababu zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Fedha hizo hazivuki maji kuja Tanzania Bara, huingia moja kwa moja kwenye akaunti kuu ya Pay Master General Zanzibar. Kwa hiyo, fedha hizo zimekwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya Mlipaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar. (Makofi)