Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Moja ya jukumu la Serikali ni kuhudumia wafungwa kwa maana ya kukwapatia huduma za msingi kama vile chakula, mavazi na matibabu:- Je, Serikali inafanya nini ili kuhakikisha huduma hizo za msingi katika Gereza la Kasulu zinapatikana kwani wana hali mbaya sana hasa kimavazi?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa zaidi ya wafungwa katika Gereza la Kasulu ni wakimbizi hali inayochangia gereza hilo kubeba mzigo mkubwa. Je, Serikali iko tayari kukaa na Shirika la UNHCR ili iweze kuchangia pesa katika Gereza la Kasulu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa miongoni mwa huduma nyingine za wafungwa ni pamoja na usafiri; na kwa kuwa gereza la Kasulu ninakabiliwa na ukosefu mkubwa wa gari la kubebea mizigo, lori la kusombea vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuni za kupikia chakula; je, ni lini Serikali itapeleka pesa kwa ajili ya kununua gari kwa ajili ya gereza la Kasulu? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba UNHCR wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za wakimbizi, lakini hata na wananchi ambao wanazunguka maeneo husika. Kwa hiyo hili jambo tunalolifanya si jambo ambalo linalotakiwa lianze sasa hivi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la gari tuna changamoto kubwa sana ya uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza, kwa hiyo kwa sasa hivi siwezi kutoa ahadi yoyote kwa sababu gari hizo hazipo; lakini zikapopatikana nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunachukua changamoto yake kama moja ya vipaumbele.