Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Seif Khamis Said Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manonga

Primary Question

MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani juu ya suala la kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Chomachankola hasa ikizingatiwa kuwa wataalam wa kilimo walikuja kufanya utafiti na kueleza mpango wa kuchimba bwawa kwa ajili hiyo pale Chomachankola?

Supplementary Question 1

MHE. SEIF K. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nipende sasa kuuliza maswali mawili madogo.
• Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa usanifu ulikwishafanyika, je ni lini sasa huu mpango kabambe utaanza kutekelezwa katika Kijiji cha Chomachankola? (Makofi)
• Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wananchi wa maeneo ya Ziba, Ndebezi, Nkinga, Mwisi, Simbo, Igoeko na Uswaya wanategemea sana kilimo cha mpunga ambapo sasa wanalima msimu mmoja na hawana scheme wala mabwawa.
Je, ni lini sasa Mheshimiwa Waziri pamoja na wataalam wako mtaweza kuzuru maeneo hayo mjionee ukubwa wa tatizo ili kuja na majawabu ambayo yataweza kutatua changamoto katika maeneo tajwa? Ahsante.

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kuliandaa na kulijibu swali vizuri sana. Sasa nijibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ni lini tutaanza utekelezaji wa skimu ya Chomachankola. Nimhakikishie tu kwamba mpango kabambe umekamilika na kuanzia mwaka ujao wa fedha tunaanza ku-mobilize fedha na hasa kwa nje na kuanza kutekeleza hiyo progamu kwa sababu hiyo programu itashirikisha taasisi nyingi sana za wadau.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mpango kabambe umeanisha maeneo yote, kwa hiyo tutakachofanya ni kuhakikisha kwanza tunajenga chanzo cha maji na baadaye ku-develop hizo skimu ili tuhakikishe kwamba maeneo yote yanayofaa kwa kilimo cha mazao ya aina yote yanalimwa kwa umwagiliaji. (Makofi)