Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Norman Adamson Sigalla King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA KING aliuliza:- Mwaka 2016 - 2018 bei ya zao la mahindi ambayo ndiyo nguvu ya uchumi kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imeshuka sana hadi kufikia shilingi 2000 kwa debe kwenye baadhi ya Wilaya kama Ludewa na Makete. • Je, ni lini Serikali itaongeza fedha NFRA ili mahindi yanayozalishwa yanunuliwe na kuwapa ahueni wananchi? • Je, ni lini Serikali kupitia NFRA itajenga maghala katika kila Halmashauri ili kurahishisha uhifadhi wa mahindi na mazao mengine?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, nina swali moja tu la nyongeza.
Kwa kuwa maeneo yote yaliyotajwa kwa ajili ya ujenzi wa maghala hazijatajwa sehemu zile ambazo tunajua zinazalisha mahindi kwa wingi ikiwemo Wilaya ya Makete, nini kauli ya Serikali juu ya ujenzi wa ghala Makete?

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kuwatetea wananchi wake na kunihimiza kufika Makambako tarehe 3 mwezi huu kwenda kuangalia hali ya ununuzi wa mahindi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizingatia jibu langu la msingi niliyataja maeneo mbalimbali ambayo Serikali inakwenda kujenga maghala ya kuhifadhia mahindi kuanzia ya Halmashauri mpaka ya wakala wetu wa hifadhi. Moja ya sehemu hiyo ni Makambako; Makambako ni Makao Makuu ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inajumuisha Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya pamoja na Songwe. Eneo analotoka Mheshimiwa Mbunge ni Makete, ni eneo la Mkoa wa Njombe na ni sehemu ya hii Makambako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili eneo la Makambako ndiyo tunakwenda kujenga ghala kubwa kuliko sehemu yoyote Tanzania; maghala haya matatu tunayoenda kujenga yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 60,000 kwa mwaka. Maana yake tukiongeza na uwezo wa sasa wa ghala lile tani 39,000 tutakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 99,000. Hii maana yake maeneo ya mikoa yote hiyo miwili hususani Mkoa wa Njombe ambako lipo Makao Makuu na Wilaya ya Makete tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi mahindi kwa mwaka ujao Desemba. (Makofi)