Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Seif Ungando

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa kwenye harakati za Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 alikubali kuwa mlezi wa Shule ya Sekondari Mahenge na akaahidi kutatua tatizo sugu la maji katika shule hiyo. Je, ni lini Serikali itaipatia shule hiyo maji safi na salama kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais Mstaafu?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwanza tunashukuru Kibiti tumechimbiwa visima 12 vikiwa katika Kijiji cha Mtunda, Nyamisati, Mahege, Mlanzi na Kivinja A. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha miundombinu hiyo ili wananchi hawa wapate maji safi na salama?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwamba je, sasa Naibu Waziri yupo tayari kuongozana na mimi kwenda katika Wilaya Mpya ya Kibiti, ili kujionea adha ya wananchi wanayopata na ukizingatia sasa hivi Kibiti ni salama?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Mbunge binafsi, Mbunge anafanya kazi nzuri sana. Nataka nimhakikishie wananchi wa Kibiti kwamba Mbunge wao anatosha mpaka chenji inabaki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge sisi Wizara yetu ya Maji tumeona haja ya kuusaidia Mji wa Kibiti na tumechimba visima 12. Kubwa sisi tunataka tukamilishe miundombinu ile, ili wananchi wale waweze kupata maji. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi jukumu letu katika kuhakikisha miradi ile tunaikamilisha kwa wakati, ili wananchi wake waweze kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu suala la mimi kwenda Kibiti. Nataka nimhakikishie kwa kuwa, sasahivi Kibiti ni salama, mimi kama Naibu Waziri niko tayari kwenda kuambatana naye kuzungumza na wananchi.