Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Primary Question

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza:- Serikali iliweka Wilaya ya Mkinga kuwa miongoni mwa Wilaya za kipaumbele kujengewa Chuo cha VETA. Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi ya kujenga Chuo cha VETA Wilayani Mkinga?

Supplementary Question 1

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu haya hayaridhishi hasa ukizingatia kwamba ahadi hii ya Serikali ni ya muda mrefu takriban miaka saba sasa. Pale Mkinga tunategemea uwekezaji mkubwa sana wa kiwanda kikubwa cha cement, uwekezaji wa takriban dola bilioni tatu. Uwekezaji ambao utavutia takriban viwanda 11. Sasa kwa muktadha huo, nini mkakati wa Serikali wa kuleta Chuo cha Ufundi pale Mkinga ili vijana waweze kupata stadi zitakazowawezesha kuingia kwenye uchumi huu wa viwanda? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wenzetu wa Singapore kwa kutambua changamoto ya ajira katika nchi yao, wametumia mfumo ambao umewawezesha kuondoka kwenye tatizo, mfumo wa ku-link mafunzo ya VETA na maeneo ya kimkakati ya uzalishaji (industrial park) je, Serikali iko tayari kujifunza kutoka kwa wenzetu ili tuondokane na tatizo tulilonalo? (Makofi)

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa sana Mheshimiwa Kitandula anaposema jibu langu la msingi halijamridhisha kwa sababu kwa kweli kwa miaka mitatu sasa amekuwa kila wakati yupo Wizarani akifuatilia ujenzi wa VETA ya Wilayani kwake Mkinga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupitia Bunge lako Tukufu nimhakikishie Mheshimiwa Kitandula kwamba tayari mchakato wa kujenga Chuo cha VETA Mkinga umefikia katika hatua za mwisho. Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Dubai inayoitwa Planet Core iko katika hatua za mwisho za kuingia mkataba wa PPP ili waweze kujenga vyuo kumi nchini kikiwepo Chuo cha VETA cha Mkinga. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba awe na subira kidogo tu kwa sababu kile ambacho amekuwa akitafuta kwa muda mrefu sasa kiko mbioni kutekelezwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.