Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jamal Kassim Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magomeni

Primary Question

MHE. JAMAL KASSIM ALI aliuliza:- Idadi kubwa ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo ili kujipatia mapato na moja kati ya changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo ni ukosefu wa mitaji ya kuwezesha shughuli zao kuwa na ufanisi na tija zaidi:- Je, Serikali ina mikakati gani kupitia Benki ya Kilimo kuwasaidia wananchi hao kupata mitaji ya kilimo?

Supplementary Question 1

MHE. JAMAL KASSIM ALI: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumpongeza Naibu Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya. Pamoja na majibu mazuri aliyotoa nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa vile Sera ya Serikali yetu ni kwenda kwenye uchumi wa viwanda na viwanda vingi vimekuwa na uhaba wa malighafi ambazo zinatokana na bidhaa za mazao na kupelekea viwanda vyetu kuagiza malighafi kutoka nchi za nje, je, Serikali ina mkakati gani kupitia benki hii sasa kuanza kukopesha wakulima wakubwa ambao wataongeza uzalishaji wa malighafi ambazo zitaenda kulisha viwanda vyetu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, benki hii imekabiliwa na uhaba wa mtaji, ilianzishwa kwa mtaji wa shilingi bilioni 60 lakini lengo lake lilikuwa kufikia mtaji wa shilingi bilioni 80. Je, nini commitment ya Serikali kuhakikisha kwamba mtaji wa benki hii utaongezeka ili kusaidia kuongeza idadi ya wakopeshaji lakini pia kuongeza single borrow limit kama ambavyo maelekezo ya BOT yameelekeza?

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Jamal, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nieleweke kwamba Benki yetu ya Kilimo ni benki ya kisera tofauti na zile benki zingine za kibiashara. Benki hii ya Kilimo ambayo ni ya kisera ilikuwa imeundwa kwa makusudi maalum kwa ajili ya kusaidia wakulima wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake hili kuhusu wakulima wakubwa, ni kweli hawa Niche Farmers kwa maana ya wakulima wakubwa sera na sheria yetu ni katika kuhakikisha kwamba na wenyewe wanafanya na wakulima wadogo kwa maana ya outgrowers ili kuweza kuongeza ule mnyororo wa thamani katika mazao yetu ya kilimo. Katika Benki yetu ya Kilimo ni kwamba wenyewe tunaposema ni benki ya kisera ni kwa sababu riba yao ni ndogo zaidi kutoka asilimia 8 hadi asilimia 12 kulingana na wakati ule ambao wao wenyewe wanaomba kama ni muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ambao unafika miaka 15.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kuhusu mkakati pamoja na mtaji, kama nilivyosema hii ni benki ya kisera kwa maana hiyo Serikali imewekeza asilimia 100 katika benki hii ili kuhakikisha kwamba inawakomboa wakulima. Mheshimiwa Spika, ahsante.