Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. SAADA MKUYA SALUM (K.n.y. ANGELINA ADAM MALEMBEKA) aliuliza:- Baadhi ya Wabunge wa Majimbo walihama Vyama vyao na kujiunga na vyama vingine hivyo Chaguzi Ndogo zikafanyika na Chama cha Mapinduzi kikashinda Majimbo hayo:- (a) Je, ni nini hatma ya Wabunge wa Viti Maalum walioingia Bungeni kupitia asilimia za Majimbo yao ya Uchaguzi? (b) Kwa kuwa Chama cha Mapinduzi kimeongeza idadi ya Majimbo zaidi, je, ni lini Wabunge wa Viti Maalum wapya wa CCM kupitia Viti Maalum wataingia Bungeni?

Supplementary Question 1

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake, hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa utaratibu huu uliopo hivi sasa na tendency tunayoiona, je, Serikali haioni inanyima fursa uwakilishi wa wanawake hapa Bungeni kutokana na ongezeko la Viti hususani kwa upande wa Chama cha Mapinduzi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu mwongozo huu unatokana na sheria, sasa ni lini Serikali italeta mabadiliko haya ya sheria hapa Bungeni ili tuweze kurekebisha tuone kwamba idadi ya wanawake inaongezeka hapa Bungeni? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Saada Mkuya, kwa pamoja, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya awali, msingi wa mgawanyo wa Viti Maalum unatokana na Ibara ya 78(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo ada, pamekuwepo na marekebisho mbalimbali ya Katiba kutokana na mahitaji. Inapotokea haja ya kufanyika hivyo basi Serikali tutaona umuhimu wa kuona jambo hili kwa uzuri zaidi ili iweze kubadilishwa kuendana na mazingira ya wakati husika, lakini kwa hivi sasa msingi unabaki kuwa Ibara ya 78(1) ya Katiba ndiyo ambayo inatuongoza.