Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA (K.n.y. MHE. HALIMA J. MDEE) aliuliza:- Baadhi ya maeneo katika Jimbo la Kawe yanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama kwa kipindi kirefu. Maeneo kama Kata ya Mabwepande (Mtaa wa Mbojo, Mabwepande, Kinondo); Kata ya Makongo (Mtaa wa Changanyikeni na baadhi ya maeneo ya Mtaa wa Makongo Juu); Kata ya Wazo, Mbweni na Mbezi Juu na changamoto hii sugu ilitarajiwa kupungua na kumalizika kabisa baada ya mradi mkubwa wa maji wa Ruvu Chini kukamilika ambao kwa sasa tayari umeshakamilika. • Je, mikakati ya usambazaji maji pamoja na mabomba katika maeneo ambayo hayana mtandao wa mabomba ikoje ili kutatua kero husika? • Je, ni miradi gani inayotarajiwa kutekelezwa, muda wa utekelezaji, gharama za kila mradi na nani anayewajibika katika utekelezaji?

Supplementary Question 1

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri na kwamba kweli ujenzi wa matenki unaendelea, lakini kuna maeneo mengine ambayo ni korofi kama Mabwepande, Kijiji cha Mbopo na maeneo mbalimbali ya Kata ya Mbezi ikiwemo Mtaa wa Ndumbwanji. Ni lini sasa Serikali itatia mkazo kuhakikisha maeneo hayo yanapatiwa maji kwa haraka sana kwa sababu kumekuwa na shida?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Manispaa ya Iringa na Iringa kwa ujumla inategemewa kuwa ni kitovu kikubwa cha utalii wa Kusini na Manispaa ya Iringa imebakiza asilimia nne za upatikanaji wa maji. Je, ni lini sasa hizo asilimia nne zitaisha ili watalii watakapofika kule wasipate matatizo wanapokwenda katika maeneo yale? (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya jitihada kubwa sana kuondoa tatizo la maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa hali ya upatikanaji ipo katika asilimia 75 lakini yapo maeneo ambayo hayana maji. Serikali kwa kuona hilo sasa kuna mradi ambao unatekelezwa kutoka Mpiji – Tegeta
(a) Bagamoyo lakini Mbezi mpaka kwa kaka yangu Mheshimiwa Mnyika katika kuhakikisha inatatua tatizo la maji.
Kwa hiyo, mpaka mkataba huu utakapokuwa umesainiwa na kupata kibali kutoka Benki ya Dunia tutatekeleza kwa wakati ili wananchi wa Dar es Salaam waweze kupata maji safi, salama na yenye kuwatosheleza.
Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kulishukuru Bunge lako Tukufu, katika bajeti yetu ya Wizara ya Maji tumepitishiwa kiasi cha shilingi 727,345,000,000. Katika fedha hizo tutauangalia Mji wa Iringa katika kuhakikisha tunaondoa tatizo la maji. Ahsante sana.