Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maria Ndilla Kangoye

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIA N. KANGOYE aliuliza:- Tanzania kuna mashirika makubwa yasiyo ya Kiserikali ambayo yanaisaidia sana Serikali katika kuwahudumia wananchi hasa wanawake misaada ya Kisheria. Mfano wa Mashirika haya ni TGNP, LHRC, WILDAF, TAWLA, lakini yanafanya kazi kwa kutegemea ufadhili wa wahisani kutoka nchi za nje:- (a) Je, ni lini Serikali itatenga asilimia kidogo ya pato lake kuyapatia ruzuku mashirika haya kama Serikali inavyotoa kwa vyama vya siasa? (b) Je, ni lini Serikali itayahamasisha mashirika na makampuni ya ndani nayo kuona umuhimu wa kuingia nayo mikataba ya ushirikiano ili kutoa huduma kwa kiwango kikubwa zaidi?

Supplementary Question 1

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza napenda kusema kwamba nasikitika sana kwani sijaridhishwa na majibu ya Naibu Waziri, ukizingatia kwamba ametoa mfano mmoja mmoja kwa kila kipengele cha swali langu wakati NGOs zipo nyingi ndani ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nijielekeze katika kuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa vijana na wanawake ndio engine ya maendeleo ya nchi yetu: Je, ni lini Serikali itaanza kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya wanawake na vijana kabla ya utoaji wa milioni 50 kwa kila kijiji? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa zipo Taasisi za Kitanzania ambazo zimekuwa zikisaidia vijana wanaoathirika na madawa ya kulevya na tasisi hizi zimekuwa ni chache kulingana na wingi wa vijana hawa, je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia taasisi hizi ili ziweze kupanuka na kusaidia vijana wengi zaidi?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maria Ndila Kangoye, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwenye taasisi hizi mbalimbali?
Serikali haina tu mipango, Serikali imeshaanza utekelezaji wa anachokisema kupitia taasisi mbalimbali. Wizara mbalimbali zinatoa elimu kwenye vikundi mbalimbali ambavyo wanafanyanavyo kazi, lakini pia sisi kwenye Wizara yetu specifically tuna Benki ya Wanawake ambayo imeanzisha utaratibu wa kuanzisha siyo matawi ya benki, lakini kuanzisha vikundi kwenye kila mkoa ambapo wanawake wajasiriamali na hata wanaume na vijana wanapewa elimu ya ujasiriamali na pia wanawezeshwa mitaji kupitia utaratibu ambao wamejiwekea.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, kwamba Serikali ina mpango gani kuhusu kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana? Tayari Serikali inafanya jambo hilo. Namwomba Mheshimiwa Mbunge asiwe na shaka na kazi inayofanywa na Serikali kwa kuwa inafanywa kwa ustadi wa hali ya juu.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIA N. KANGOYE aliuliza:- Tanzania kuna mashirika makubwa yasiyo ya Kiserikali ambayo yanaisaidia sana Serikali katika kuwahudumia wananchi hasa wanawake misaada ya Kisheria. Mfano wa Mashirika haya ni TGNP, LHRC, WILDAF, TAWLA, lakini yanafanya kazi kwa kutegemea ufadhili wa wahisani kutoka nchi za nje:- (a) Je, ni lini Serikali itatenga asilimia kidogo ya pato lake kuyapatia ruzuku mashirika haya kama Serikali inavyotoa kwa vyama vya siasa? (b) Je, ni lini Serikali itayahamasisha mashirika na makampuni ya ndani nayo kuona umuhimu wa kuingia nayo mikataba ya ushirikiano ili kutoa huduma kwa kiwango kikubwa zaidi?

Supplementary Question 2

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Kwa kuwa wanawake wengi sana wanaoishi vijijini hasa katika Mkoa wetu wa Iringa, wamekuwa wakipata shida sana wanapotafuta msaada wa kisheria; na kwa kuwa mashirika haya mengi yako mijini.
Je, Serikali inawasaidiaje wananchi ambao wanakaa mbali na miji ili angalau hata kupeleka mobile elimu ili waweze kufikiwa?

Name

Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tanga Mjini

Answer

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli wanawake wengi walioko vijijini wanakabiliwa na changamoto ya kupata msaada wa Sheria, lakini nataka nimthibitishie kwamba kwa sasa hivi Waziri wa Katiba na Sheria tayari ameshaleta mapendekezo ya Kutunga Sheria ya Msaada wa Kisheria ambapo itahakikisha msaada wa kisheria unapatikana kwa wananchi wote wenye mkahitaji, wakiwemo wanawake walio vijijini. Kwa hiyo, ni suala ambalo tayari Serikali ya Awamu ya Tano inalifanyia kazi na tunataka kumuahidi kwamba ndani ya siku chache tutakuwa na sheria, hivyo wanawake wataweza kupata.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya pili; tayari tunazo NGOs mbalimbali ambazo zinafanya kazi ya kutoa Msaada wa Sheria kwa wanawake, ikiwemo Chama cha Wanasheria Wanawake na Chama cha Wanawake Wanahabari. Kwa hiyo, tunazo taasisi mbalimbali ambazo zinatoa msaada wa sheria kwa wanawake.