Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA (K.n.y. MHE. LUCY S. MAGERELI) aliuliza:- Mradi wa Maji wa Kimbiji na Mpera chini ya Kampuni ya Serengeti Limited ulianza Machi, 2013 na Desemba 2016 ulitarajiwa kukamilisha visima 20 ambavyo vitawahudumia wananchi wa Kigamboni na Mkuranga. Waziri wa Maji na Umwagiliaji Oktoba, 2016 akitembelea mradi huo na kuagiza ukamilike kwa wakati uliopangwa vinginevyo kampuni ingelipa gharama za ucheleweshaji lakini hadi leo mradi huo haujakamilika:- (a) Je, Serikali imeshawajibisha kampuni hiyo kwa kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo? (b) Je, ni lini mradi huo utakamilika ili kuondoa adha kwa wananchi wa Kigamboni ambao wengi wao wanatumia maji ya visima vifupi ambavyo sio salama?

Supplementary Question 1

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, ninayo maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Lucy Magereli. Swali la kwanza, wakati wa Bajeti ya Wizara ya Maji, Kamati ya Kisekta na Waheshimiwa Wabunge walipendekeza kwamba tuongeze Sh.50 katika mafuta ili kupata fedha ya kupeleka maji vijijini na mijini ili kumaliza tatizo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni je, kwa maelezo ya majibu ya Wizara hii, na mradi umeanza tangu mwaka 2013 ulipaswa kuisha mwaka 2016, huu ni mwaka 2018; si kwamba kuna upungufu wa fedha ndiyo maana mradi huu unasuasua? Kwa hiyo ningeomba nipate kauli ya Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa mjadala wa Wizara ya Maji, ukurasa wa 56, mradi huu wa visima virefu wa Kimbiji na Mpera vinahusu pia Jimbo la Ukonga Kata ya Msongola, Chanika, Buyuni, Pugu, Kitunda na Ukonga. Sasa ningeomba nipate kauli ya Serikali hapa wamesema watu wa Kigamboni kuna mradi mbadala wa kupeleka maji katika eneo hilo. Nini kauli ya Serikali kuwasaidia watu wa Ukonga Kata ambazo nimezitaja, mradi wa dharura ili waweze kupata maji safi na salama? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kumpongeza Naibu Waziri kwa majibu mazuri kabisa. Nami pia niseme kwamba nimeshukuru Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo moja kwa moja kwamba, sasa Wizara ya Maji ni eyes on, hands on kwenye halmashauri. Baada ya kauli hiyo kabla ya tarehe 30, nitafanya kikao kikubwa na Wahandisi wa Maji wote katika halmashauri ili tupeane mwelekeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nichukue nafasi hii kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Kwanza kabisa kuhusu Visima vya Kipimbi na Mpera, tumefanya kazi kubwa sana, nampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, tumekuwa naye na tulikutana na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa ambao wamekubali kwamba watatusaidia fedha kwa ajili ya kuweka miundombinu ya maji Wilaya ya Temeke pamoja na Kigamboni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Serikali inaendelea na mazungumzo. Kwa hiyo, suala la fedha halina shida tena ni utaratibu tu, baada ya kusaini financial agreement mambo yote yatakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna shida yoyote kwamba mradi umechelewa kwa sababu hii Sh.50, hapana, kwa sababu hii Sh.50 kwanza inaelekezwa moja kwa moja vijijini. Hii ni miradi mikubwa ambayo inatekelezwa kwa fedha kutoka Central Government.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, tushakamilisha mazungumzo na Serikali ya Ufaransa na tukapata hiyo fedha, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hii ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi, itahakikisha kwamba maeneo yote ya Dar es Salaam yanapata maji safi na salama pamoja na kata alizozisema, pamoja na hata kwa Mheshimiwa Zungu kule Ilala, tunahakikisha kwamba tunakamilisha ili wananchi waweze kupata maji safi na salama sambamba na kuondoa majitaka.