Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Jasmine Tiisekwa Bunga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Vyuo Vikuu

Primary Question

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA aliuliza:- Milima ya Uluguru ni chanzo kikubwa sana cha maji katika mito na vijito vingi ambavyo husaidia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa maji safi na salama katika Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. Hata hivyo, kutokana na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na ujenzi holela, kilimo na ufugaji, mito hiyo imeanza kukauka hivyo kusababisha adha kubwa ya upatikanaji wa maji kwa wananchi:- Je, Serikali ina mipango gani ya kimkakati ya kuilinda milima hiyo isiendelee kuharibiwa na kuhakikisha miti iliyokatwa inapandwa mingine ili kuhifadhi vyanzo vya maji?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante Naibu Waziri kwa majibu mazuri, napongeza Serikali kwa mpango mzuri ambao wameueleza. Hata hivyo, kama alivyozungumza kwenye majibu yake, ameonesha kabisa kwamba milima hii ina ikolojia ya pekee, bioanuai adhimu, lakini kuna mifuko ambayo imeanzishwa kwa Hifadhi ya Tao la Mashariki na utekelezaji wa mradi wa miaka mitano kuanzia 2016 – 2021 pamoja na vijiji vinavyozunguka, napongeza kwa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sasa kwenye hii Milima ya Uluguru, kwa sababu uhifadhi sio lazima uwe pale kwenye chanzo, maana yake pamoja na hills yaani vijilima vyake. Lakini ukiangalia kwa sasa hivi pale Manispaa ya Morogoro ile milima iliyozunguka kuanzia maeneo ya Kilakala, Bigwa, Kigurunyembe na Pangawe ambayo hapa kuna vyanzo vikubwa sana vya maji ambao wakazi hawa wote niliowataja wa Bigwa, Kigurunyembe na Kola tunategemea maji kutoka kwenye milima hii, lakini mito hii imekauka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inasababishwa na uharibifu mkubwa ambao unaendelea sasa hivi kwenye milima hii ya Bigwa, Kigurunyembe, Pangawe ambapo sasa watu wanajenga kwa kasi kubwa sana ndani ya ile misitu, wanakata ile misitu yaani… (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kwa sababu pia pale kuna Mbega wale weupe na ndege ambao ni adimu. Je, Serikali imechukua hatua gani kusimamisha na kudhibiti ujenzi huu holela ambao unaendelea katika milima hii ambayo ni vyanzo vikubwa vya maji? Ahsante. (Makofi)

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa tarehe 5 Aprili, nilifanya ziara ya kukagua uharibifu wa mazingira kwenye maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyasema. Maeneo hayo ndiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge kwa juhudi kubwa aliweza kuyafuatilia na wakashirikiana na Serikali ya Mkoa na Serikali ya Wilaya wakawaondosha wale watu ambao walikuwa wanajenga kiholela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maagizo ambayo niliyatoa kwa Manispaa ya Morogoro ni kuhakikisha kwamba wanatengeneza mpango mkakati wa namna ambavyo watashughulikia uharibifu huu wa mazingira. Mheshimiwa Tisekwa ile climate change strategy niliyomwahidi, nitampatia hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo ningependa Wabunge waelewe, masuala ya uharibifu wa mazingira au uchafuzi wa mazingira wamekuwa wakidhani ni vyanzo vya maji kuviharibu au kukata miti, ni pamoja na upigaji wa makelele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi hapa, Hajji Manara wakati anatangaza kwamba mechi yao na Simba wacheze ili mapato yale yatakayopatikana waweze kuisaidia Yanga watu walipiga makelele sana, nikaulizwa haya makelele kwa mujibu wa mazingira yana mahusiano gani. Nikasema kwa mujibu wa kifungu cha 106, makelele yanazuiwa lakini yale makelele ya kushabikia kama matamko ya Hajji Manara yale yanaruhusiwa kwa mujibu wa mwongozo. Ahsante sana. (Makofi)