Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mary Pius Chatanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. MARY P. CHATANDA aliuliza:- Umeme katika Mji wa Korogwe uliingia miaka 50 iliyopita ukitokea kwenye mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Mji wa Hale kilometa 30 toka Mji wa Korogwe. Umeme huo ulikusudiwa kupelekwa kwenye mashamba makubwa ya mkonge na chai na ili kuupata umeme huo kwa Mji huo ilibidi upite kwenye mashamba ya mkonge Magunda, Kwashemshi na kwenda kwenye mashamba ya chai ya Ambangulu na Dindira:- Je, Serikali haioni ni wakati muafaka Mji wa Korogwe na viunga vyake kuunganishwa na Gridi ya Taifa?

Supplementary Question 1

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba niulize swali la nyongeza.
Kwa kuwa amesema kwamba umeme umeunganishwa katika Gridi ya Taifa kule Hale; na kwa kuwa Korogwe imekuwa umeme unakatika mara kwa mara. Je, ni lini umeme utakoma kukatika ili kusudi wananchi wa Korogwe Mjini waweze kufanya shughuli zao za biashara pamoja na shughuli nyingine bila kuwa na kukatika kwa umeme?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mary Chatanda kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa katika Mkoa mzima wa Tanga umeme unakuwa ukikatika mara kwa mara na suala la kukatika umeme mara kwa mara siyo kwa Mkoa wa Tanga peke yake, lakini sasa hivi tunachofanya, tunafanya marekebisho ya miundombinu yote katika Mikoa karibu yote. Kati ya mikoa yote, Mkoa wa Tanga tumeupa kipaumbele. Tunafanya marekebisho ya transfoma pamoja na chanzo cha umeme cha Hale.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti hii inayokuja, tuombe sana Waheshimiwa Wabunge, tunadhani mtaipitisha; tumetenga pesa kwa ajili ya kurekebisha mitambo hiyo. Kwa hiyo, Mkoa wa Tanga na Korogwe mtapata umeme wa uhakika baada ya bajeti hii.

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Primary Question

MHE. MARY P. CHATANDA aliuliza:- Umeme katika Mji wa Korogwe uliingia miaka 50 iliyopita ukitokea kwenye mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Mji wa Hale kilometa 30 toka Mji wa Korogwe. Umeme huo ulikusudiwa kupelekwa kwenye mashamba makubwa ya mkonge na chai na ili kuupata umeme huo kwa Mji huo ilibidi upite kwenye mashamba ya mkonge Magunda, Kwashemshi na kwenda kwenye mashamba ya chai ya Ambangulu na Dindira:- Je, Serikali haioni ni wakati muafaka Mji wa Korogwe na viunga vyake kuunganishwa na Gridi ya Taifa?

Supplementary Question 2

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa na mimi niuliza swali la nyongeza. Mji wa Maramba una tatizo kubwa sana la kukatika kwa umeme kama ilivyo Mji wa Korogwe. Je, Waziri atatuhakikishia kwamba katika mipango hiyo anayoizungumza ina-consider vile vile Mji wa Maramba?

Name

Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Vijijini

Answer

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la kukatikakatika umeme, sababu mojawapo ni miundombinu kuwa inasafirisha umeme mdogo ambao haulingani na matumizi. Kwa hiyo, project kubwa kabisa ambayo tuna nyingine tunaizindua mwezi wa tisa ni kutoka kwenye miundombinu inayosafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kwenda 400.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndugu zangu wa Tanga, hii inatoka Dar es Salaam inapita Tanga ikielekea Arusha halafu kuna nyingine inatoka Iringa, Dodoma kuelekea Shinyanga. Ni lazima tuwe na umeme mwingi ndiyo tutakomesha ukatikaji wa umeme mara kwa mara na hilo tatizo linatatuliwa. Ahsante.