Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:- Wilaya ya Serengeti ni Wilaya yenye mbuga kubwa ya wanyama inayotambulika duniani na kupokea watalii wengi, lakini imekuwa kama kisiwa kwa kusahaulika kuunganishwa na barabara ya lami itokayo Makutano ya Musoma mpaka Mto wa Mbu:- Je, ni lini barabara ya lami ya Musoma – Mugumu mpaka Mto wa Mbu itakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ya Makutano – Mugumu – Mto wa Mbu imetengewa fedha kuanzia mwaka 2012 - 2013 ili kujenga kilometa 50 kuanzia Makutano mpaka Sanzate.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyoongea, tangu mwaka 2013, hii ni 2016, hata kilometa moja ya lami haijawahi kukamilika. Sasa kama kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa ni miaka mitano...
Miaka mitano kilometa 50 haijakamilika. Uki-cross multiplication it will take 45 years kukamilisha kilometa 452.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali, nataka Mheshimiwa Waziri awaambie wananchi wa Serengeti, ni lini watakamilisha ujenzi wa lami kuanzia Makutano mpaka Mto wa Mbu?
Swali la pili, ninavyoongea, sasa hivi hakuna mawasiliano kwenye hii barabara, imekatika! Daraja la Mto Robana limekatika. Serikali iko tayari kuji-commit sasa hivi kupeleka hela zikajenge yale madaraja ambayo yamebomoka?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha kwa kusimamia kwa ukamilifu Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imekusudia na imeweka barabara hii katika Ilani yake na tunaanza kuitekeleza kwa mwaka ujao wa fedha ukiacha kile ambacho kimeshafanyika katika kipindi kilichopita. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka ujao wa fedha, bajeti yetu itakapofika, Waheshimiwa Wabunge naomba muikubali ili tuweze kutekeleza Ilani hii ya Chama cha Mapinduzi. Katika barabara hii shilingi bilioni 12 tumezitenga kwa ajili ya kujenga kipande hiki anachokiongea na shilingi bilioni nane tumeitenga kwa ajili ya kujenga upande wa pili wa Arusha ambayo nimeiongelea.