Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Uharibifu wa mazingira kwenye Msitu wa Chome (Shengena) umeleta athari kubwa ya uchafuzi wa maji hasa katika Mito mikubwa ya Yongoma na Saseni; mito hiyo kuanzia kwenye vyanzo vya maji imebadilika rangi na kuonesha rangi yenye matope. Kwa kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ilikanusha kwamba hakuna ushahidi unaoonesha kwamba athari za mazingira katika msitu huo zinatokana na uchimbaji wa madini ya bauxite. • Je, Serikali ipo tayari kuunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha uharibifu huo katika Msitu wa Shengena? • Je, Serikali ipo tayari kuwapatia wananchi miti ya asili inayoongeza maji ili kudhibiti upungufu wa maji katika vyanzo vya maji mito hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kama Mheshimiwa Waziri atafuatilia na naamini ataunda hiyo Kamati maana najua bado mazingira ni machafu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la nyongeza ni kwamba; kwa kuwa hii mito mikubwa minne ya Yongoma, Saseni, Hingilini na Nakombo imejaa magogo ambayo yameletwa kutoka misituni na hivyo kufanya maji yatuame na yasiwafikie watu walioko mabondeni.
Je, Waziri atatusaidiaje au Serikali itatusaiaje kufundisha wananchi na kuwapa vifaa ili waweze kufanya usafi wa ile mito yaani Kiingereza wanaita dredging ili watoe yale magogo ili maji yaweze kufikia wananchi walioko bondeni?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba Mito ile ya Hingilini, Saseni, Yongoma pamoja na Nakombo ni kweli imeathiriwa na shughuli za kibinadamu yakiwemo hayo mdgogo aliyoyasema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kifupi tutauma tena timu ya wataalam ili waende waone ukubwa wa lile tatizo na baada ya kuona ukubwa wa lile tatizo watatupa taarifa ambayo tutawashirikisha wananchi wenyewe katika maeneo yale ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha juu ya matatizo haya ambayo yanafanyika katika vyanzo vya maji. Kwa hiyo, Mheshimiwa Kaboyoka usiwe na wasiwasi na kama utakuwa tayari kuambatana na mimi nitakapokuja kule, mimi nitakuwa tayari pia kuambata na wewe, ahsante sana.

Name

Martha Moses Mlata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Uharibifu wa mazingira kwenye Msitu wa Chome (Shengena) umeleta athari kubwa ya uchafuzi wa maji hasa katika Mito mikubwa ya Yongoma na Saseni; mito hiyo kuanzia kwenye vyanzo vya maji imebadilika rangi na kuonesha rangi yenye matope. Kwa kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ilikanusha kwamba hakuna ushahidi unaoonesha kwamba athari za mazingira katika msitu huo zinatokana na uchimbaji wa madini ya bauxite. • Je, Serikali ipo tayari kuunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha uharibifu huo katika Msitu wa Shengena? • Je, Serikali ipo tayari kuwapatia wananchi miti ya asili inayoongeza maji ili kudhibiti upungufu wa maji katika vyanzo vya maji mito hiyo?

Supplementary Question 2

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Iramba, Tarafa ya Ndago, Kata ya Ndago kwenye Magereza ya Ushora ambayo yana “A” na “B”, Ushora pamoja na Mirungu kulikuwa na msitu mkubwa na miti mikubwa ambayo ilikuwa ni chakula cha tembo lakini wafungwa wale wamemaliza ile miti hadi wale wanyama wamehama kule. Waziri ananiambia nini kuwapelekea miti wale wafungwa wakapande waturudishie msitu wetu? Ahsante.

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Martha Mlata, alipokuwa kwenye Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira alikuwa anazungumzia sana juu ya ukataji wa miti hovyo kwenye Gereza la Ushora. Mimi niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wote na niwakumbushe kwamba suala kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa kifungu namba sita cha Sheria Namba 20 ya mwaka 2004 sote tunawajibika kufanya hivyo. Tuendelee kuhakikisha kwamba zile taasisi ambazo ziko kwenye maeneo yetu yakiwemo magereza, shule, hospitali wahakikishe kwamba wanatumia nishati mbadala kama ambavyo Mheshimiwa Waziri alivyoelekeza.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Martha Mlata kupitia swali lako hili, naendelea kuzitaka taasisi zote ambazo tulishazielekeza wasiendelee kukata miti kwa ajili ya nishati, waendelee kutumia nishati mbadala na katika siku ya Mazingira Duniani ambayo tunaanza tarehe 30 Mei mpaka tarehe 5 Juni, 2018 kutakuwa na maonesho ya…

…watu mbalimbali katika kutumia nishati mbadala. Mheshimiwa Martha Mlata nitakuwa tayari kuambatana na wewe kwenda Gereza la Ushora, ahsante sana.

Name

Yussuf Salim Hussein

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chambani

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Uharibifu wa mazingira kwenye Msitu wa Chome (Shengena) umeleta athari kubwa ya uchafuzi wa maji hasa katika Mito mikubwa ya Yongoma na Saseni; mito hiyo kuanzia kwenye vyanzo vya maji imebadilika rangi na kuonesha rangi yenye matope. Kwa kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ilikanusha kwamba hakuna ushahidi unaoonesha kwamba athari za mazingira katika msitu huo zinatokana na uchimbaji wa madini ya bauxite. • Je, Serikali ipo tayari kuunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha uharibifu huo katika Msitu wa Shengena? • Je, Serikali ipo tayari kuwapatia wananchi miti ya asili inayoongeza maji ili kudhibiti upungufu wa maji katika vyanzo vya maji mito hiyo?

Supplementary Question 3

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Waswahili wanasema usipoziba ufa utajenga ukuta. Imekuwa ni tatizo linaloendelea na ni maneno kila siku yanazungumzwa kuhusiana na uharibifu wa vyanzo vya maji na hususani Chemchemi.
Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi wote wanaozunguka maeneo ya vyanzo vya maji ili kuhakikisha kwamba wao ndio walinzi lakini hao hao wawe ndiyo watunzanji wa mazingira wa maeneo yale?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sera yetu hii ya Taifa ya Hifadhi ya Mazingira pamoja na Sheria ya Mazingira tayari Mheshimiwa Waziri alishatoa miongozo na maelekezo kwa Halmashauri zote 185 Tanzania watuletee orodha ya vyanzo vyote vya maji ikiwa ni pamoja na changamoto. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge tuko katika harakati za kuhakikisha kwamba tunaweka mikakati ya utoaji wa elimu kwa wananchi ambao wako kwenye vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kutangazwa kwenye Magazeti ya Serikali. Ahsante sana.