Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

ASHA MSHIMBA JECHA aliuliza:- Mradi wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Vijijini (MIVARF) katika Mkoa wetu wa Kusini Unguja umeweza kuwakomboa wananchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha mawasiliano ya barabara na kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi. Kwa kuwa mradi huu umeonesha mafanikio na wananchi wamehamasika. Je, Serikali ipo tayari kuwaongezea mitaji na mafunzo wananchi hao ili waweze kufikia malengo yao?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Kwanza niipongeze kupitia mradi huu, kwa kweli imejitahidi sana kwa haya waliyoyasema na wanachi tayari wameonesha matunda na uzalishaji umekuwa. Mheshimiwa Jenista ni shahidi alikuja kutembelea maeneo ya Kongoroni na akajionea jinsi gani wananchi walivyoimarika katika uzalishaji wa kilimo cha ndimu. Kwa taarifa niliyonayo sasa hivi kwamba mitambo ya kiwanda cha ndimu tayari imefika na tayari imejaribiwa bado ufungaji tu naamini kazi hiyo itafanyika. Kwa kuwa mradi huu umeonesha maendeleo makubwa na bado kuna maeneo mengine yanahitaji mradi kama huu.
Je, Serikali kupitia mradi iko tayari kuendelea kwa yale maeneo mengine ambayo hayajafikiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swala langu la pili elimu haina mwisho; kwa kuwa vikundi hivi vineonesha mwelekeo mzuri na bado vingali na changamoto ya kuyafikia masoko lakini hata kuongeza ujuzi wao.
Je, mradi huu uko tayari kuendelea na vikundi hivi ili kufikia lile lengo la kuondokana na uchumi mdogo na kuingia uchumi wa kati katika ulimwengu huu wa sasa hivi wa viwnda? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kama Serikali kupitia mradi huu utaendelea kuyafikia maeneo ambayo hayafikiwa. Nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba mradi huu ambao una lengo la kwenda kurekebisha miundombinu ya barabara na masoko maeneo ya vijijini na kuongea tija katika mazao unaendelea kuwanufaisha Watanzania, na kadri ambavyo miradi inazidi kuibuliwa basi tutayafikia pia na yale maeneo ambayo bado hayaguswa kutokana na maelekezo na mwongozo wa mradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili Mheshimiwa Mbunge amezungumza kuhusu suala la mafunzo na kuviendeleza vikundi ambavyo vimeshapatiwa fedha kupitia mradi huu. Kwa mujibu wa utaratibu wa mradi huu wa MIVARF miradi hii ikisha ibuliwa katika halmashauri kazi sisi tunayoyanya ni kuwezesha na baadaye kazi ya kuendelea kuvilea vikundi hivi inabaki katika halmashauri husika. Kwa hiyo niendelee tu kumuomba Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa sababu tayari mradi huu umeshafanya kazi yake eneo la uendelezaji wa vikundi hivyo pia na wenyewe kwa nafasi yao waweze kushiriki kuhakikisha kwamba vikundi hivi vinakuwa endelevu na viweze kuleta tija kwa Mtanzania. (Makofi)