Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Mohamed Chuachua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- • Je, ni lini Serikali itaondoa kabisa malalamiko yanayotokana na makato, rushwa, uwazi na matatizo mengine yaliyopo katika mfumo mzima wa ununuzi wa zao la korosho? • Je, ni lini Serikali itaondoa utaratibu wa wakulima kulipwa mara mbili na badala yake walipwe pesa zao mara moja na wasubiri bonus baadae? • Ni lini Serikali itadhibiti usambazaji wa pembejeo kwa watu ambao siyo wakulima wa korosho?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Mheshimiwa Naibu Waziri kwanza nikupongeze kwa sababu ulipopata tu Unaibu Waziri ulikuja Masasi na ukatembelea wakulima wa korosho. Kwa hiyo, changamoto za wakulima wa korosho unazifahamu. Nina maswali mawili yanyongeza.
Swali la kwanza; kwa kuwa hadi sasa wakulima wa korosho waliouza korosho zao katika msimu uliopita wanadai fedha zao takribani zaidi ya shilingi milioni 90 katika Jimbo langu tu la Masasi kwa hiyo fedha hizo ni zaidi ya shilingi milioni 90. Je, ni lini Serikali itahakikisha wakulima hawa wamelipwa fedha zao?
Swali la pili, lini Serikali sasa itaingiza sulphur ambayo itauzwa kwa wakulima kwa sababu tunafahamu wakulima wananunua sulphur kwa mwaka huu. Sasa lini Serikali itaingiza sulphur hiyo na kuisambaza kwa bei nafuu kwa wakulima wetu, kwa sababu kwa sasa begi moja ya sulphur imefika shilingi 70,000 mpaka shilingi 80,000? Ahsante sana.(Makofi)

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa umahiri wake wa jinsi anavyofuatilia wakulima wa zao la korosho katika Mkoa wa Lindi na Mtwara hususan katika Jimbo lake la Masasi na ninaomba kwa maana hiyo nijibu maswali yake yenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nikianza na lile la (a) ni kweli wakulima wa zao la korosho wanadai Serikali na naomba niseme tu kwamba Mkoa mzima wa Lindi na Mtwara ikiwemo Masasi wakulima wanadai zaidi ya shilingi bilioni 5.770 Serikali naomba niseme tu kwamba katika Mkoa wa Lindi wataanza kulipwa mwezi huu mwishoni na vilevile katika Mkoa wa Mtwara watalipwa mwezi ujao mwishoni.
Mheshimiwa Spika, nikija katika swali lake la (b) kuhusu suala zima la pembejeo, ni kweli kabisa tunaelewa kwamba kumekuwa na changamoto kubwa sana ya pembejeo katika zao zima la korosho na ninaomba nilitaarifu Bunge lako tukufu kwamba kwa upande wa sulphur habari njema ni kwamba Serikali tumeagiza tani 35,000 na lita 520 za viwatilifu na tunategemea mwezi huu Aprili awamu ya kwanza itafika na awamu ya pili itafika mwezi ujao mwishoni.
Mheshimiwa Spika, ninaomba niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba pembejeo hizi kuanzia sasa zitanunuliwa kwa bei ambayo kwa upande wa sulphur haijazidi shilingi 40,000; vilevile kwa upande wa vile viwatilifu haitazidi shilingi 30,000; kwa maana hiyo ni habari njema haitakuwa shilingi 70,000 au 80,000 kama Mheshimia Dkt. Chuachua alivyosema bali itakuwa shilingi 40,000. Ahsante. (Makofi)