Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silafu Jumbe Maufi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Serikali ilitoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Namanyere Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi hadi Ninde yenye urefu wa kilometa 40 lakini hadi sasa ujenzi wa barabara hiyo bado haujakamilika kwa muda mrefu sasa. (a) Je, ni lini Serikali itachukua hatua kwa kufuatilia na kuchunguza matumizi ya fedha zilizotolewa na kuchukua hatua ili ujenzi wa barabara hiyo uweze kukamilika? (b) Je, ni lini wananchi wa Ninde wataondokana na changamoto ya barabara?

Supplementary Question 1

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu suala hili, bahati nzuri mwenyewe anayezungumza ni ametoka Mkoa wa Rukwa, kwa hiyo, barabara hii anaifahamu vilivyo. Akina mama wengi na watoto wanapata shida kwenye barabara hii wanapokuja kupata huduma ya afya Namanyere.
Napenda kuiuliza Serikali, je, ina mpango gani kwa hivi sasa kwa sababu tupo katika kipindi cha bajeti kuweza kutenga fedha za kutosha kuikamilisha hii barabara badala ya kuendelea kutengeneza maeneo korofi kila mwaka hadi mwaka na kuonekana kana kwamba ni mradi wa Serikali? (Makofi)
Swali la pili, ninapenda kuiomba Serikali ijaribu kuona hizi barabara zetu za Bonde la Lake Tanganyika na Bonde la Lake Rukwa, barabara hizi ni tata, zinahitaji matengenezo yaliyokamili kama vile Kitonga na inavyoelekea kutumika katika kipindi chote cha mwaka mzima.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba barabara hii ina changamoto kubwa maana kuna maeneo ambayo kuna milima mikubwa sana na azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba wananchi wa Ninde wanapata barabara inayoweza kupitika kwa vipindi vyote.
Mheshimiwa Spika, kabla ya hapo ilikuwa hakuna barabara kabisa na ndiyo maana Serikali kwa kulitambua hilo ikaanza kutenga kiasi cha shilingi milioni 350 na maeneo yaliyokuwa korofi zaidi ilikuwa ni maeneo ya madaraja. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ilimradi madaraja yameshajengwa ambayo ndiyo yalikuwa ni changamoto kubwa sana, nia na azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba maeneo yaliyobaki yataweza kutengenezwa kwa kadri bajeti itakavyokuwa inaruhusu.
Katika swali lake la pili, ameongelea Ukanda wa Ziwa Rukwa. Sifa ya Ukanda wa Ziwa Rukwa na hii barabara aliyoitaja ya kwenda Ninde hazina tofauti sana na Mbunge, Mheshimiwa Malocha amekuwa akiipigia kelele sana na kwa mara ya kwanza Serikali imesikia kilio chake na barabara hii inaweza kuimarishwa ili iweze kupitika katika kipindi chote.

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Serikali ilitoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Namanyere Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi hadi Ninde yenye urefu wa kilometa 40 lakini hadi sasa ujenzi wa barabara hiyo bado haujakamilika kwa muda mrefu sasa. (a) Je, ni lini Serikali itachukua hatua kwa kufuatilia na kuchunguza matumizi ya fedha zilizotolewa na kuchukua hatua ili ujenzi wa barabara hiyo uweze kukamilika? (b) Je, ni lini wananchi wa Ninde wataondokana na changamoto ya barabara?

Supplementary Question 2

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza.
Kwa kuwa mwaka huu tumebarikiwa mvua lakini mvua hizi zimeleta madhara sehemu mbalimbali na kuharibu miundombinu ya barabara.
Ningependa kujua, je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na majanga haya ya barabara hususani zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA)? (Makofi)

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ahsante.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Serikali tumejipanga na kama ilivyo kawaida kila mwaka tunatenga fedha kwa ajili ya kutibu dharura kwa maana ya emergency, kwa sasa hivi maeneo mengi ambayo barabara hazipitiki tumewaagiza Meneja wa TANROADS washirikiane na TARURA ili kuweza kuokoa sehemu hizi ambazo hazipitiki na Wizara tunaendelea kuratibu na kufuatilia ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma wanapita kwenda kwenye shughuli zao za maendeleo. Ahsante.